MISTARI YA WIMBO HUU

Aah Kev
We taking over Suma Mnazaleti na Stamina
Aah (Mnazaleti mi natokelezea)

Mistari imejaa ubabu hadi mababa wanaamkia
Huyu bibi kaitaka rap atakimbizwa hadi atalia
Kama kila awamu walikula awamu ya nne wamekomba
Madogo wameiteka hadhira watu wazima game mtasanda
Utanganyika una kivuli cha ujinga tabu na shida
Kijana akivaa msuli basi ujana ushampoteza
Nauli imepanda kidogo Kigamboni watu wanalia
Bush ashabanwa ule mchongo soon wataanza kuogelea
Maduka ya dawa za siri wateja wakubwa madada
Ukihonga honga kiakili usije ukadhani ulipendwa
Money iligeuka power ghafla Gadaffi akaachia nchi
Wageni wanatesa wazawa Kariakoo imekosa weusi
Mi nahitaji namba kumi sio moja ntakosa stand
Viongozi wameanza na umimi hili taifa wanaliweka bond
Tamaa ikizidi uwezo mwili lazima utumike
Shida ukii-use kama kigezo hiyo sketi lazima ishuke

Tatizo lilikuwa muda sasa tumeshika mishale
Agano jipya sie mabudha bye bye agano la kale
Moro na Kigoma majembe ndo tuko mjini
(Umetusoma hujatusoma sikiliza track kwa makini sema yeah)
Stamina na Mnazaleti
Haina kupoa kila mchongo unajiseti
(Sema yeah Stamina na Mnazaleti)
Ah aah ah aah

Hii sio system ya Madilu haina shobo kwa mademu
Kingunge mtafute mwiru Ngombare ashasanda game
Mistari sukari guru hii lazima itakunogea
Ila mashaka yatakudhuru usijaribu ku-compare
Mzungu akijichubua ujue moyoni ana uafrika
Dogo usikimbilie kukua omba kubarehe kifikra
Vesti ya mcheza sumo Betina lazima ikupwaye
Kitambo kama Gurumo Mabeste nicheki baadae
Sio kila mwembamba ni model sharo usiishi kiisidingo
Na kifo ndo mwisho wa nyodo jipange uache maringo
Nimezaliwa jangwani kivipi unitishie ukame
Mkulima rudi shambani hii ndo mundu ya Machame
Kabwela mwenye kitambi bepari utamtesa nani
Kokote mi kwangu kambi Anthony unipe ramani
Sadaka ni sadaka ila zaka iende kwa Isaka
Mamlaka yenye dhihaka nasaka mpaka waraka ah

Tatizo lilikuwa muda sasa tumeshika mishale
Agano jipya sie mabudha bye bye agano la kale
Moro na Kigoma majembe ndo tuko mjini
(Umetusoma hujatusoma sikiliza track kwa makini sema yeah)
Stamina na Mnazaleti
Haina kupoa kila mchongo unajiseti
(Sema yeah Stamina na Mnazaleti)
Ah aah ah aah

Ndevu zingekuwa ndo hekima Osama asingeujua ugaidi
Na mvi sio utu uzima jipange uache ukaidi
Juisi haipashwi wala mstimu haumwagiliwi
Bubu acha magumashi chunga usimfokee kiziwi

Wanataja walikotokea ili waongeze mashabiki
Mi kwetu ndo mwisho wa reli ukifata level hizi hufiki
Ustaa Bongo unapeperuka ka trouser bwanga ya Loketo
So ukipata weka jenga ili kesho wasikuite Kapeto

Ukikumbuka ulikotokea masai utachana chupi
Na usiogope kupotea kama njia huikumbuki
Darasa bila dawati gonga nyundo ya kilimo
Mchungaji tumia torati shetani akija na mzimu

Yeah
Upendo penda unapopendwa usipopendwa stress zinatosha
Upendo wa mke umezidi ndugu mama mkwe mpaka kasusa
Cha maana ndo chenye maana kwa wenye maana bila dhana
Wachanaji sio wale wa jana wanaochana leo wana laana

Tatizo lilikuwa muda sasa tumeshika mishale
Agano jipya sie mabudha bye bye agano la kale
Moro na Kigoma majembe ndo tuko mjini
(Umetusoma hujatusoma sikiliza track kwa makini sema yeah)
Stamina na Mnazaleti
Haina kupoa kila mchongo unajiseti
(Sema yeah Stamina na Mnazaleti)
Ah aah ah aah

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI