MISTARI YA WIMBO HUU

Niliapa ukiondoka mpenzi
Ntaondoka nawe
Sikuahidi kukufuta machozi
Bali ntalia nawe
Tamani hata kugeuka mpenzi kunitazama
Hutaki Awena
Basi kama na kosa kwako nililofanya
Nieleze Awena
Chozi langu la thamani unaliacha lianguke ehee
Tuliopanga zamani ina maana si chochote eh?
Utamu wa mapenzi niujuao mi na we
Kipenzi changu Awena
Utamu wa mapenzi niujuao mi na we
Rudisha moyo Awena
Iweje penzi langu kwako unalikatisha
Iweje ehee!
Iweje penzi langu kwako unalikatisha
Ina maana tunda langu basi utamu umekwisha, baby?!

Labda ungesema mapema kuwa penzi langu hulihitaji Awena
Kuliko kuondoka wakati moyo wangu bado unakuhitaji Awena
Utamu wa mapenzi niujue mi na we
Kipenzi changu Awena
Utamu wa mapenzi niujue mi na we
Rudisha moyo Awena
Labda ungesema mapema kuwa penzi langu hulihitaji Awena
Kuliko kuondoka wakati moyo wangu bado unakuhitaji Awena
Utamu wa mapenzi niujue mi na we
Kipenzi changu Awena
Utamu wa mapenzi niujue mi na we
Rudisha moyo Awena

Nahisi kuna mtu amekubadilisha mawazo
Kama rafiki zako wasiopenda penzi lako
Uliwaeleza kitu ambacho ulihisi ungepata afadhali mpenzi
Nahisi kuna mtu amekubadilisha mawazo
Ama rafiki zako wasiopenda penzi lako
Uliwaeleza kitu ambacho ulihisi ungepata afadhali mpenzi
Maneno matamu ulionipa chumbani
Huku kichwa chako umelaza kifuani
Machozi yakikutiririka mashavuni
Kwamba hutoniacha mimi labda utoweke duniani iih
Umeniacha kipindi ambacho sitaraji mpenzi
Moyo wangu bado unalihitaji lako penzi
Utaniacha kipindi ambacho sitaraji mpenzi
Moyo wangu bado unalihitaji lako penzi

Rudi Awena
Rudi mpenzi iihihi hii
Rudi Awena
Rudi mpenzi basi ehee hee

Labda ungesema mapema kuwa penzi langu hulihitaji Awena
Kuliko kuondoka wakati moyo wangu bado unakuhitaji Awena
Utamu wa mapenzi niujue mi na we
Kipenzi changu Awena
Utamu wa mapenzi niujue mi na we
Rudisha moyo Awena
Labda ungesema mapema kuwa penzi langu hulihitaji Awena
Kuliko kuondoka wakati moyo wangu bado unakuhitaji Awena
Utamu wa mapenzi niujue mi na we
Kipenzi changu Awena
Utamu wa mapenzi niujue mi na we
Rudisha moyo Awena

Labda ungesema mapema kuwa penzi langu hulihitaji Awena
Kuliko kuondoka wakati moyo wangu bado unakuhitaji Awena
Utamu wa mapenzi niujue mi na we
Kipenzi changu Awena
Utamu wa mapenzi niujue mi na we
Rudisha moyo Awena
Labda ungesema mapema kuwa penzi langu hulihitaji Awena
Kuliko kuondoka wakati moyo wangu bado unakuhitaji Awena
Utamu wa mapenzi niujue mi na we
Kipenzi changu Awena
Utamu wa mapenzi niujue mi na we
Rudisha moyo Awena

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI