MISTARI YA WIMBO HUU

Ulianza wewe wakaja waimbaji na wabana pua
Wale mwewe franga wawindaji wakatusua
Kwakuwa wanajua mshikaji unaishi kwa miko
Na zako itikadi ziko kimziki na sio mshiko
Kama haileti hela basi haimake sense
No sweat kisela mie nikakomaa tu na lako penzi
Siku-sound garbage au kuchange suddenly
Mie ni mjeshi so naweza fight savagely
Hip Hop ya ukweli ukapigwa radioni
Sometimes malaika wa heri nao hutembelea motoni
Penzi ni kipofu na anayemuona halioni
Sikuwa na hofu mama alinipenda tangu nikiwa tumboni
I started young I made my mother’s womb a drum
My umblirical chord a guitar muhoji aliyenizaa
Bongo Flava mzuri kiasi Hip Hop we ndo my queen
My first my last and everything in between

Nasema mimi na we tangu long long time
Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii fame
Cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream
Bongo Hip Hop
Bongo Hip Hop

Nasema mimi na we tangu long long time
Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii fame
Cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream
Bongo Hip Hop
Bongo Hip Hop

Kama kukupenda wewe ni dhambi basi shetani yu nami
Na kamwe sintonyea kambi ili niwabambe dukani
For a million little pieces naweza kum-con Oprah ka James Frey
Na watasema sitishi wakati wanaogopa nisitokee
Waufuate mkumbo huu wa wasomi wa midundo na mistari
Ukiwa na nyundo mkononi ni rahisi kupigilia msumari
Sio tu Bongo mpaka ng’ambo hakuna uhuru wa habari
Kuna uhuru wa mwenye chombo mitambo na mwenye mali
Kujifanya hawasikii haiwasaidii wala haiwajengi
Unachosema ni kamwe IPP haitompinga Mengi
Unawakumbusha wazazi wa uswazi chati ya uteja imeingia
Na mapusha wanauza drugs ili walishe familia
Mbaya kuhifadhi fuvu la mtu ndani ya kabati
Mbaya zaidi ni kuwa na ndugu halafu kichwa maji
Amka bongo lala Hip Hop sio ufala ni lazima uifate
Uaminifu ni kama mshahara fanya kazi ili uupate

Nasema mimi na we tangu long long time
Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii fame
Cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream
Bongo Hip Hop
Bongo Hip Hop

Nasema mimi na we tangu long long time
Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii fame
Cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream
Bongo Hip Hop
Bongo Hip Hop

Mapenzi ya sikuhizi bila kugombana yanakua hayana stimu
Pia ni ruksa kushikana lakini sio kushikiana simu
Inanipa wazimu kusikia kimwana haujaachana na Hasheem
Na bado mnawasiliana una mpango wa kuchanganya timu
Nakupenda Hip Hop ndo maana ninarap ile mbaya
Naspit fire bila Hennessy au kula kaya
I want my art to be my legacy kabla sija-retire
Waanze nigwaya hawa enemies anyways ni hayo tu
Beef huletwa na wivu na wivu sio Hip Hop
MC nayetaka beef amlete maza ‘ake kwa strip club
Bongo Flava ananipima kama nimeiva kimasomo
Anagundua mie ni dreamer pia ni believer zaidi ya Common
Cha ajabu uni-tempt ili nikuache Hip Hop
Anaahidi atanipa good sex wewe unanipa true love
Hajui who’s next wewe unanipa tu mashavu
Nikipaa anaumia anatamani nishuke chini
Nami sikutamani ustaa ustaa ulinitamani mimi
Nilichohitaji ni kuitumia hii sanaa ili nishee na nyinyi
Hii zawadi niliyopewa na Mpaji ninayemuamini
Mpaji aliyenivika taji ilimradi in charge ni win
Na ninaamini kuna muda huongea kwa kupitia mimi
Na hunisamehe ninapokosea ni vyema mkanizoea nyinyi
Naweza kuona unachotaka au atakachonionyesha
Nikitoa ngoma wanaitaka wanaipata ’cause wewe ni special

Nasema mimi na we tangu long long time
Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii fame
Cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream
Bongo Hip Hop
Bongo Hip Hop

Nasema mimi na we tangu long long time
Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii fame
Cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream
Bongo Hip Hop
Bongo Hip Hop

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU