MISTARI YA WIMBO HUU

Nahisi nina bahati mbaya kipi nilichokosea
Nikijaribu kutafuta shida ndo zinakolea
Mifukoni hali mbaya sio kama najitetea
Ile pesa ya kusuka mbona nilikuletea
Mawazo yani yananikolea
Nikupe nini usijepotea
Ndubura yani inanyong’onyea
Lilinde penzi lisije teketea
Vitunguu mboga za majani laki tano kwenye genge
Nyama tu nikupe million kwani unapika kenge
Si jana tu nimelipa pochi na doti za vitenge
Viatu juu ulivyojumua kama una duka mwenge

Chuma ulete
Chuma ulete
Usiwe chuma ulete
Nisije kubadili jina nikakuita chuma ulete
Chuma ulete mama chuma ulete
Usiwe chuma ulete
Nisije kubadili jina nikakuita chuma ulete

Pesa sio nguvu za milundi kunyanyua jiwe juu chini
Tukitoka unakuja na kundi gharama zote juu yangu mimi
Unanasa pesa kama gundi sasa mimi nitumie nini
Kila siku kushona kwa fundi kama mpambaji wa shuhulini
Eti nguva inaita mara mapande sita
Mshazali umeshika hakuna fashion inakupita eeh
Juzi ulikunja ndita wataka mchele tani sita
Mama mbona unanitisha kwani unafutulisha

Mawazo yani yananikolea
Nikupe nini usijepotea
Ndubura yani ninanyong’onyea
Lilinde penzi lisije teketea
Vitunguu mboga za majani laki tano kwenye genge
Nyama tu nikupe milioni kwani unapika kenge
Si jana tu nimelipa pochi na doti za vitenge
Viatu juu ulivyojumua kama una duka Mwenge

Chuma ulete
Chuma ulete
Usiwe chuma ulete
Nisije kubadili jina nikakuita chuma ulete
Chuma ulete mama chuma ulete
Usiwe chuma ulete
Nisije kubadili jina nikakuita chuma ulete

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU