MISTARI YA WIMBO HUU

Dear gambe umefanya maisha yangu yayumbe
Mi nimpambe wako leo nimekutumia ujumbe
Mi ndugu yako nipe ukweli usinifumbe
Uwepo wako karibu vp unafanya ni yumbe
Kila muda kwene friji unajipoza,
Mi domo zege nikisha kutumia natongoza
Nalewa usiku kucha jua lina chomoza
Nasindikiza na supu asubuhi njema unaniongoza
We ni nani unaiyendesha hii akili
Ninikiwa na mawazo unanitoa stress nisifikiri
Ukiwa mezani chupa kadhaa sijiwezi
Mpaka mtaani washanipa jina jingine la mlevi
Unafanya nafubaa mi mwenzako
Hadi kazini naiba chapaa nije kwako
Dear gambe mitaa ipo ukweli wako
Nakila ugomvi wa baa kwanini chanzo ni chako

I wanna know
Umenipa nini
I don’t know
Sikuachi kwa nini
I wanna know
Umenipa nini
I don’t know
Sikuachii kwa nini eeh

Unafanya ndoa nyingi zinavunjika
Hasi-chanya we na msosi nikichanganya na tapika
Haukatai kila mteja anae kuarika
Unafurahi na ubaridi wa maji unachirizika
Likitokea tatizo we ndo kimbilio
Nakutinga nakua muongeaji bila mpangilio
Nasahau kinga tamaa ndo kimbilio
We ni funda la ziada unaniumbua mi mwenzio
Unalainisha koo kifikra unanibembeleza
Unani-control sijasoma naongea hadi kingereza
Ushaniweza nani aliyekutengeneza
Na nini aliwaza nawe ni mbaya kwa wasiojiweza
Sa najinyea nanilikunywa kwa furaha
Najikojolea unaniathiri na ninatoa chapaa
Dear gambe mitaa ipe ukweli wako
Nakila ugomvi wa baa kwanini chanzo ni chako

I wanna know
Umenipa nini
I don’t know
Sikuachi kwa nini
I wanna know
Umenipa nini
I don’t know
Sikuachii kwa nini eeh

Dear gambe unanichanganya sana
Unamajina mengi mpaka ya mbuga za wanyama
Nashangaa mengine yanatia kinyaa
Mfano mzuri ni gongo, chimpumu hata chang’aa
Kwenye ubongo umetawala kila sector
Niukweli siwezi kuwa nawe bila pesa
Watu wengine wana kula ada kisa wewe
Unawafanya wanasahau ibada
Na juzi juzi tu nimepata habari
Kuna mwana ulikua nae ameshapata ajali
Dear gambe nikweli unanichosha
Napenda kuwa nawe ila nyumbani mboga wanakosa
Nawaza jinsi gani ntakuacha
Mpaka wazalendo wa dini baadhi kwako wamedata
Hakuna utata, poa sasa najikata
Kapuku nikizipata ntakufata

I wanna know
Umenipa nini
I don’t know
Sikuachi kwa nini
I wanna know
Umenipa nini
I don’t know
Sikuachii kwa nini eeh

I wanna know
Umenipa nini
I don’t know
Sikuachi kwa nini
I wanna know
Umenipa nini
I don’t know
Sikuachii kwa nini eeh

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI