MISTARI YA WIMBO HUU

Ditto nashika peni kwenye fani najongea
Nasema kwa makini sikia nachoongea
Dunia ina mambo
Dunia ina mambo toka kitambo
Dunia hii imejaa chuki na masimango
Ona sasa braza men chupuchupu kupewa kisago
Kakopa nguo kwenye malipo kageuka mbogo
Akina dada mnaorukia mapenzi bado wadogo
Anamuita dogo na kweli mdogo
Lakini la ajabu anatembea na vigogo
Shule kwaacha kwa tamaa ya vitu vidogo
Wizi unapamba moto dunia inatoa somo
Na je ni lini ukimwi utafika kikomo?
Utafika kikomo pale utakapoacha ngono
Naitwa Ditto oh, naitwa Ditto kutoka Bongo Record

Dunia ina mambo
Ingia kwenye mitaa, wazushi wamezagaa
Majungu yamejaa, dunia ina mambo
Duniani ukilemaa hupati kitu kabisa
Hupati kitu kabisa

Dunia ina mambo
Ingia kwenye mitaa, wazushi wamezagaa
Majungu yamejaa, dunia ina mambo
Duniani ukilemaa hupati kitu kabisa
Hupati kitu kabisa

Kweli dunia ina mambo
Tena dunia ina mambo, vijambo toka kitambo
Kama ukifata mkumbo, yaani ukimuiga tembo
Oh oh utakwenda kombo
Bora unyamaze tu, ujifanye hauna makuu
Ukipata unakula buku, ukikosa unauchuna tu (chuna tu)
Kama mi na Majani, KO na Juma Mchizi
Tuna-rap, tuna-blaze, tunafanya mziki kazi
Sio mapenzi, sio ubitozi
Mbona unanitazama? Ama unazishangaa rasta?
Zangu mi nyeusi tii, au labda unadata
Unashangaa baba T navyonata kisanii
Namna hii kwenye hii beat ya P? Hamna noma eh
Kushangaa mara moja, ya pili uniulize swali
Ukishangaa mara ya tatu ntahisi unataka shari
Utafeli, kama washikaji flani
Sorry, vinabo flani
Waliokuwaga na mi muda flani, sio zamani
Wenye tabia za kike wanachonga chonga pembeni
Wanachonga kila leo, kuhusu mimi na Kandeo
Au mimi na Mkama Deo, ambao kwa mchango wao
Ndo mimi nikapiga bao, amani kwao
Watu hao wenye uchungu, uchungu na damu yangu
Tangu tangu na tangu nilipozimwa na mzungu
Kwenye uzinduzi wangu
Kisha nikapakaziwa nimedhurumu wenzangu
Bado alikuwa na mimi katika kumuomba Mungu
Kama Professor Jay, Jay Moe na Brother K
Amani kwao watu hao, hata na Majani eh

Dunia ina mambo
Ingia kwenye mitaa, wazushi wamezagaa
Majungu yamejaa, dunia ina mambo
Duniani ukilemaa hupati kitu kabisa
Hupati kitu kabisa

Dunia ina mambo
Ingia kwenye mitaa, wazushi wamezagaa
Majungu yamejaa, dunia ina mambo
Duniani ukilemaa hupati kitu kabisa
Hupati kitu kabisa

Kwenye vilinge watu hawawazi maendeleo
Ukichunguza wanawaza flani kala nini leo
Kwa jinsi navyoona ni ukosefu wa upeo
Ebwana, majungu na fitina hayaleti maendeleo
Mtu mwenye busara anatafuta muelekeo
Anawaza, siku zinavyokwenda atapataje maendeleo
Awe na maisha bora mara kumi zaidi ya leo
Ni sakata la mwaka, dada kamtaka kaka
Kaka nae katamani kasema, “ondoa shaka”
Hali ya maisha ngumu, pesa haipatikani
Mchana na jioni ya mboga haionekani
Utafanya nini na jua kali mpaka mfukoni
Wengine wakipata hela misele kwenye komoni
Anazuga na bia moja kutoa harufu mdomoni
Mabinti nao wanaozeshwa bado wadogo
Mali kwenye familia zinaleta zogo
Wajomba na shangazi wanataka japo kidogo
Ah, dunia ina mambo
Wajomba na shangazi wanataka japo kidogo
Ah kitu kidogo tu

Dunia ina mambo
Ingia kwenye mitaa, wazushi wamezagaa
Majungu yamejaa, dunia ina mambo
Duniani ukilemaa hupati kitu kabisa
Hupati kitu kabisa

Dunia ina mambo
Ingia kwenye mitaa, wazushi wamezagaa
Majungu yamejaa, dunia ina mambo
Duniani ukilemaa hupati kitu kabisa
Hupati kitu kabisa

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI