MISTARI YA WIMBO HUU

Mziki wenu ana ana doo
Unafanya mshindwe hata kufikiri
Kutwa kwenye vioo kuliko kuandika mashairi
Hip Hop mizuka yakujuza usivyojua
Hivi mziki wenu unanuka
Mbona mnabana pua

Swali lako kwangu halina jibu
Ulichouliza hakinihusu
Sema kama unanijaribu au dogo una-force beef
Hapa kwangu pakavu sitaki upuuzi
Maswali ya kupana pua na poda muulize Dimpoz

Aa haa hamna cha maana kutwa kuwaimbia wasichana
Unalikuta libaba lizima eti oh nakula ujana
Haziingii akilini na hazielimishi jamii
Sa nimjue wa nini aliyemwaga pombe ya nanii Eeh

Okay Professor Jay bwana mdogo si unamjua
Hata baba ‘ako nyumbani naimani anamtambua
Kwa nyimbo za kuelimisha we pimbi kaa kimya
“Kamili Gado” imetoboa ali-change mtu mzima

Kwani huko kwenu vipi

Aah huku kwetu fresh
Tuna manyumba tuna magari tuna cash
Kwani huko kwenu vipi

Aah huku kwetu poa
Machizi tunachana sana ila mnabebwa hadi mnaboa
Kwani huko kwenu vipi

Huku kwetu fresh
Kwani huko kwenu vipi

Aah huku kwetu safi

Huko kwenu vipi

Huku kwetu fresh
Harakati zinaendelea kwetu stress sio kesi

Mnajifanya mnafanya ngumu wakati hamna majukumu
Wengi wenu wala ndumu na bado mnaishi kwenu
Usibishane na mimi kwanza we bado unasoma
Shoo zenu bei rahisi hata kwa bia nyie mnafanya

Hip Hop inahitaji kichwa sio kunywa mchuzi wa pweza
Blaza huku kwetu ulifichwa umesepa sababu ya kumezwa
Ama kweli nimeamini wanawake mkiwezeshwa mnaweza
Kama umenishindwa mimi je Fid Q utamuweza

Kwanza hamtambui kwamba huu mziki ni kazi
Na ndo maaana mnakatazwa na wazazi
Unafanya mziki mwaka wa kumi huna hata bajaji
Nyie sio wasaniii ni wasindikizaji

Huko kwenu mnajua waganga sababu mnapeana stress
Ndo maana hadi nyimbo vamba mtaani zinakuwa the best
Blaza ushaachia siti so punguza kujisifu
Huku viumbe tunaachia hit bila hata kumtaja Chief

Kwani huko kwenu vipi

Aah huku kwetu fresh
Tuna manyumba tuna magari tuna cash
Kwani huko kwenu vipi

Aah huku kwetu poa
Machizi tunachana sana ila mnabebwa hadi mnaboa
Kwani huko kwenu vipi

Huku kwetu fresh
Kwani huko kwenu vipi

Aah huku kwetu safi

Huko kwenu vipi

Huku kwetu fresh
Harakati zinaendelea kwetu stress sio kesi

Kwa ku-post picha Insta hilo mnaongoza
Utasikia huu mjengo wangu mpya kumbe umepanga unajiongeza
Nasikia daily mko gym eti mnatanua vifua
Wakati mkirudi makwenu wengi wenu mnajichubua
Ebo

Mnajifanya mnakaza huku mnakufa njaa
Hakuna mnachopata zaidi ya sifa kwenye mitaa
Kwanza mnatudhalilisha kutwa mnapiga vizinga
Umarekani mwingi mpaka mnakula unga

Si bora sisi unga kuliko nyie mapu***
Hana style hamna swagg wala hamjui kutunga
Kwa kuongeza sifuri kwa hilo mnaujasiri
Hata video ya milioni 2 utasikia milioni 200
Sh*t

Bwa’ mdogo ongea na mimi mbona unawasema watu
Wataje kwa majina ka kweli unafanya Hip Hop
Kwanza umekula au unaanzisha tu mgogoro
Kabla hatujafika mbali una nauli ya kurudi Moro

Kwani huko kwenu vipi

Aah huku kwetu fresh
Tuna manyumba tuna magari tuna cash
Kwani huko kwenu vipi

Aah huku kwetu poa
Machizi tunachana sana ila mnabebwa hadi mnaboa
Kwani huko kwenu vipi

Huku kwetu fresh
Kwani huko kwenu vipi

Aah huku kwetu safi

Huko kwenu vipi

Huku kwetu fresh
Harakati zinaendelea kwetu stress sio kesi

Anha kama hupati unachopenda
Penda unachopata au sio
Mwisho wa siku hii ni biashara
Inabidi mwisho wa siku tupendane sisi kwa sisi
Au sio
Don’t take it personal man
(Seductive Records)
Au sio Mambo yataongeleka au sio
Tutagombana mwisho wa siku Bongo Flava na Hip Hop
We all teame
Stamina Nay Wa Mitego T-Touch au sio
Take it easy homeboy don’t panic
It’s just a business man
Calm down errbody
Hahaha napenda nachokisikia
I’m out

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI