MISTARI YA WIMBO HUU

Kaa mbali
Kaa mbali kaa mbali kaa mbali wee
Kama upaja mdogo
Bwa’ mdogo kaa mbali wee
Kaa mbale kaa mbali wee
Kaa mbali wee

Hii ni juu mpaka chini elevator flow
Wananiita mi ni soo njoo u-generate flow
Kaa unaweza wenzako hawarap wakiniona
Wakirap nawameza nawabeza
Kwenye kila beat nikirap wao hucheza so
Ukitaka battle njoo na mic na jeneza
Stosh huwa sijafi hata kwa replay
Rapper muuza sura njoo nikupe account mpaka eBay
Na hii sio Bongo Star Search hii Bongo Stars’ Bench
Mistari inailisha nyasi kwenye Bongo Star’s range
Ma-rapper wanafua mwili wachane wamekunja sura
Peace kwa Bonta sitaki tuzo nauza kura
Na-spit kama Wallace Christoph
Kwenye beat hii ni unabii so na-spit kama Kristo
Rap ndo nyumbani mic ndo mtutu kwenye army
Ma-rapper wakiniona wanafunga milango wanarap ndani
Zungusha beat washamba wachape lapa mapema
Niteme tata wasande wapate kapa
Stosh The Rap Hero chunga usibaki witness
Wenzako wakipata zero

Hii ndo tahadhari kwa ma-MC
Mi ndo simba mkali wa raundi hii
Kaa mbali wee
Kaa mbali kaa mbali wee
Kama upaja wako mdogo kaa mbali wee
Kaa mbali kaa mbali wee
Wasije wakakupiga tobo kaa mbali wee
Kaa mbali kaa mbali wee
Kama upaja wako mdogo kaa mbali wee
Kaa mbali kaa mbali wee
Ngoma yako ya kitoto

Sijaja Dar na basi la tour toka Msamvu mpaka Ubungo
Wakiniona wanabana pua wanasema nanuka tungo
Rap imenipa ulaji sijali snitch ukiongea
Kama majungu mtaji tafuta frame uuze umbea
Nikiingiza ngumu inadumu kudumu kwenye spika
Mi matata mi nawachapa si wanataka huu-haa
Naiwaza game sio demu atanisumbua
Natema rhymes vumbi mpaka wapate mafua
Mama told me ‘Don’t tired at this step forward’
Mi ni strong man black iron na-flow radi aah
Tupa shuka andaa tanzia ya mazishi
Wananiita chief cooker maana napika hadi maandishi
Zima beat nichane salamu ma-rapper fyongo
Mchana usiku wa manane silali naumiza ubongo
Nina confidence plus heavy dense man power
Ubongo unatema sense kila verse iko sawa
Wanaosema mi ni wack kwenye chart siwaoni
Shenzi type toa track iwe trash redioni
Rapper anaecheza rafu na midundo ya kila sample
Mistari ingekuwa ni uchafu hata mimi ningekuwa na dampo
Wassup

Hii ndo tahadhari kwa ma-MC
Mi ndo simba mkali wa raundi hii
Kaa mbali wee
Kaa mbali kaa mbali wee
Kama upaja wako mdogo kaa mbali wee
Kaa mbali kaa mbali wee
Wasije wakakupiga tobo kaa mbali wee
Kaa mbali kaa mbali wee
Kama upaja wako mdogo kaa mbali wee
Kaa mbali kaa mbali wee
Ngoma yako ya kitoto

Duniani ni vilio na vicheko
Zingua tukuzike kama Ubutu Seseseko
Ukitaka kuona ngumi kali tembelea Keko
Mazoezi makali jela Segerea depo
Zamani nilitamani kuwa MC
Siku hizi natamani kuwa MP
MD WhatsApp utachat na nani now umeishiwa MB
Yule anachana kama Drake
Mi nakuja kama Land Rover bila brake
Kila siku nipo mpaka kifo nakuapia
Nawakazia mpaka wanaobana wanaachia
Mlale mahali pema Ngwea na Langa
Eti nasikia Simba katembea na Yanga
Kawaida sina mood ya kuchekea makima
Najua watoto juu ya mdundo huu mtapea lazima
Nazima moto Yesu ni jibu fill in the blank
Tafuta pesa fill in the bank
Yes yes yoh bado nadunda
AKA Stereo AKA Chunda

Hii ndo tahadhari kwa ma-MC
Mi ndo simba mkali wa raundi hii
Kaa mbali wee
Kaa mbali kaa mbali wee
Kama upaja wako mdogo kaa mbali wee
Kaa mbali kaa mbali wee
Wasije wakakupiga tobo kaa mbali wee
Kaa mbali kaa mbali wee
Kama upaja wako mdogo kaa mbali wee
Kaa mbali kaa mbali wee
Ngoma yako ya kitoto

Kaa mbali

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI