MISTARI YA WIMBO HUU

You know what Kev
This is my life man
Stamina

Nimepigwa msumari wa kichwa mwili unangoja kaburi
Maisha yamenipiga picha nega zimetoka vivuli
Dunia tambala bovu nalidekia kwa shida
Jitahidi kui-solve bila kutumia four figure
Natamani nisimame ili nione magharibi
Moyo umejaa ukame kuhema unajitahidi
Macho yote yana ukungu utadhani chungu cha bibi
Nataka kumuomba mungu shetani ananzidi spidi men
Vizuri viko wapi navisaka havionekani dah
Napata makapi vinono navitamani
Sina baba sina mama sina babu sina bibi
Uchumi wangu umesimama kama behewa la itigi
Umaskini unanipodoa bila kutumia cosmetics
Daily unanizodoa unanivuta bila magnetics
Maisha yangu hayana swagga kama mmasai wa Njiro
Natamani kula burger naishia viazi vya Gairo
Dah

Leo nimepata kesho nimekosa
Ninachohifadhi maumivu tu
Life ni ngumu bado inanichosha
Nakula mbichi sili mbivu boo
Huwezi amini bado kabwela
Sina uhuru kama niko jela
Huwezi amini bado kabwela
Sina uhuru kama niko jela

Sikusoma kitajiri kichwa kimejaa madufu
Maisha hayana tafsiri usidhani yanamjua Lufufu
Naichora lami na mkaa kwa kudhani nitaona chochote
Atleast basi ningekaa nisingeitwa kiokote
Pesa imegeuka Yuda daily inanisaliti
Mishale inazidi muda utajiri unaninyima siti
Maisha kama gwaride kuna wa mwisho na wa kwanza
Ikisikika nyuma geuka wa mwisho anakuwa wa kwanza
Taifa la kichwa changu raisi wake naona kichaa
Na kitabu cha dhambi zangu kwa Mungu kimeshajaa
Ah napatwa wazimu shida zinanitia madoa
Pesa imekuwa adimu kama bikra kwa changudoa
Banda ninalofugiwa sihemi halina dirisha
Wasichana wananikimbia wananiita nyoka wa kibisa
Minasosi wangu sio wa drafti sili mpaka nijitume
Maisha yana super shaft yashanizidi nguvu za kiume
Dah

Leo nimepata kesho nimekosa
Ninachohifadhi maumivu tu
Life ni ngumu bado inanichosha
Nakula mbichi sili mbivu boo
Huwezi amini bado kabwela
Sina uhuru kama niko jela
Huwezi amini bado kabwela
Sina uhuru kama niko jela

Ushindi wangu ni wa uchafu kwenye vita ya wasafi
Kila ninaemuomba tafu anataka afanye na ulafi
Maisha ni kombolela masikini ndio mlinda kopo
Cha msingi ni kuunga tela mpaka utoke kwenye msoto
Kila jua linapozama natamani pasikuche
Hasi inageuka chanya Kapeto anageuka Sunche
Naona alama za mlango ila sioni pa kutokea
Hii pesa imetoka jando inataka kuni-babu seya
Nimegeuka konokono natembea na mzigo wa shida
Silali nimekuwa pono maisha unakwenda na mida
Shida zishanipa ustaa zaidi ya kanda ya Loketo
Tumbo umezoea njaa hadi shibe naiona mseto
Vikombe vya uaminifu nishavivunja mtaani
Na vijiko vya uhalifu nishaviweka kwenye sahani
Mi nadhani haya maisha yana ramani
Na aliyewachorea masikini peni ilimgomea njiani

Leo nimepata kesho nimekosa
Ninachohifadhi maumivu tu
Life ni ngumu bado inanichosha
Nakula mbichi sili mbivu boo
Huwezi amini bado kabwela
Sina uhuru kama niko jela
Huwezi amini bado kabwela
Sina uhuru kama niko jela

Oohh oohoo
Ona maisha sio game
Ona maisha sio game
Sio game
Oh ohh
Leo nimepata kesho nimekosa
Ninachohifadhi maumivu tu
Life ni ngumu bado inanichosha
Nakula mbichi sili mbivu boo

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI