MISTARI YA WIMBO HUU

Mswaki kagonga hii beat ka mtoto wa Dr Dre
Nilio king wa Monii street ntaingiza vocal ka B.I.G
Mi docta kama Levi, kama snare mi na-roll
Na napendwa na walevi ka neno la alcohol
Nazungumziwa maofisini kama ishu ya Sivista
Mi na gumzo hapa mjini ka dawa ya HIV
Nipo kila nyumba kama matundu ya vyoo
Na nasakwa ka vumba, kama chinga wa Kariakoo
Slow down, go up kama nimevaa laizon
Hecta zinatoa knock-out round ya kwanza ka Tyson
Punch zina double impact kama movie la Van Damme
Nami na triple react ka hasira za mmachame
Naogopwa kama mrusi kwenye vita vya mbaguu
Na mistari myeusi kama ngozi ya mjaluo
Mswaki ni my best producer, kama mchaga na chapaa
Snitch you’re the best loser ka Rwanda na ujamaa

Kila sentensi ntayoongee lazima utasikia ka, kama
Ka, ka, ka, ka-ka, ka kama
Kila mstari ntaouandika lazima utaona ka, kama
Ka, ka, ka, ka-ka, ka kama
Hata mitaa wananiita, wananiita Mr Ka, Kama
Ka, ka, ka, ka-ka, ka kama
Siku hizi mitaa kila mtu anatupia hizo ka, kama
Ka, ka, ka, ka-ka, ka kama

Sishushi mikono chini kama katuni wa konyagi
Nazidi tema madini kama mgodi wa Buzwagi
Siko chini kama uvungu, I’m so high ile kama Jah
Wajinga nawapiga virungu kama mgambo wa manispaa
Moyo wangu haujapinda kama mkono wa mwavuli
Sina hasira ka za simba japo mkali kama chui
Sipangwi kama nyanya kwenye genge la mpare
Ila na mawazo mapana ka trouser ya Pepe Kale
Si usakwa kama jezi, fighter ka Bruce Lee
Kubwa kama GB, naheshimika ka PhD
Ni kama fanani na na-hit ka Kanumba
Mi na sss, hatupatani ka konda na Kayumba
Sirushwi kama tufe, nahifadhiwa kama stanza
Sina dhambi mi mweupe ka vile Sofia Mwanza
Kuni nachochea hizi swagga ili ziwa-pain
Daily na uhuru wa kuongea kama nimemeza Zain

Kila sentensi ntayoongee lazima utasikia ka, kama
Ka, ka, ka, ka-ka, ka kama
Kila mstari ntaouandika lazima utaona ka, kama
Ka, ka, ka, ka-ka, ka kama
Hata mitaa wananiita, wananiita Mr Ka, Kama
Ka, ka, ka, ka-ka, ka kama
Siku hizi mitaa kila mtu anatupia hizo ka, kama
Ka, ka, ka, ka-ka, ka kama

Japo sija-hit kama Tupac
Ila mi ni mpishi kama Zebaki
Acha wa-copy, wamesha-note kuwa na jay kama mswaki
Nafata nyayo kama za Biggie
Dirty money kama P Diddy
Niko speed D.I.D8, D.I.D.E kama gaidi
Natoa somo kama darasa, pumzi ndefu kama za Ngasa
Nategemewa ka Dawasa, sijiuzuru kama Lowassa
Sio mtu wa F kama Pawasa
Haters kama garasa
Mi nawachanga, weka pembeni kama mademu nawatomasa
Misimamo kama za varasi
Situmishwi kama tohara
Mziki sina papara, na wala sitoi kafara
Si napendwa kama kiduku, then na-hit ka vuvuzela
Kama ni hela naunga tela, siogopi kuwa bendera
Mgumu kama bishoo, na gangster ka hardcore
Na beef na hizo pesa, I need money kuzidi more
Nawika kama jogoo, sina pozi kama kondoo
Nimeacha watangulie, wameshakuja nakaba koo

Kila sentensi ntayoongee lazima utasikia ka, kama
Ka, ka, ka, ka-ka, ka kama
Kila mstari ntaouandika lazima utaona ka, kama
Ka, ka, ka, ka-ka, ka kama
Hata mitaa wananiita, wananiita Mr Ka, Kama
Ka, ka, ka, ka-ka, ka kama
Siku hizi mitaa kila mtu anatupia hizo ka, kama
Ka, ka, ka, ka-ka, ka kama

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI