MISTARI YA WIMBO HUU

Whaat
You know what it is
(It’s your boy Leo)
Moro town baby
Duppy I gotchu hommie
Let’s go let’s do it

I’m going in
Kama mapenzi karata mi staki niitwe kibonde
Nilishindana kunyata na kinyonga mwenye mdonde
Leta sifa za mgemba matembo akakupa uchetu
Usoni ulionesha wema kumbe moyoni sepetu
Lady uliwapepeta madume bila salama
Wavuvi ukawakeketa samaki wakaleta drama
Chimbo ya vuta ndumu kila pusha anakujua
We paka wa mkaanga sumu kila chungu unafunua
Changu ulikiona butu in peace bora uka-rest
Ukatumiwa na kila mtu kama sabuni za gest
Viduku vya Baloteli ndo mtindo uliouona mia
Kumbe kijiko cha hoteli kila mteja anatumia
Nilionyesha kukupenda mpaka kula naiamini
Kumbe msafiri wa kipemba sa stendi unafata nini
Heheh sitaki siri mi mwinyi nakupa peku
Penzi lako Makirikiri kucheza nahitaji stepu
Mwenyewe ulijiona jembe kumbe mpini wako unanesa
Khanga moja ndembe ndembe laki kwako sio pesa
Mrembo gani huna huruma kama kisu cha Ngariba
Kila upepo unapovuma kigodoro kila mida
Penzi lako bandia jabulani kwenye mpira
Kwa kuwa uliitwa Maria basi ukajiona bikira
Uliacha mlango wazi wasipate tabu ya kugonga
Kwa skendo za paparazi mtaani ukawa sex-monger ah
Kwa dhana ya ujana we msichana drama
Kwa upana ukafanya sana mabwana bila ya dhana
So mama unaweza bana ukachana bila kukana
Jana ukanitukana kwa rahma nilale salama

Nilidhani Deddy one and only kumbe nilikosea
Kila unachotaka unapata bado unazingua
Lango la jiji we unapenda chapaa (chapa)
Lango la jiji we unapenda chapaa (chapa)
Lango la jiji we unapenda chapaa (chapa)
Bye bye hunifai

It’s your boy Leo
Ua waridi upendo nilinyunyuzia
Ila makusudi ukajitahidi kuchakachua dear
Lango la jiji pita kila raia
Dada poo gwiji mwaka wa pili ume-disappear here
Mwendo kasi kiuchumi bado unadidimia
Mradi shule hutaki na uchumi wako wanautumia
Ma-superstar mafataki wanadandia
Kiroho safi kabwela baki ni mimi ntakwambia
Cheza namki wakati na hela inaingia
Muonekano safi wa nafsi kinyume na tabia
Choma penzi kwa pesa fukara wa hisia
Unavutia mtu akigusa amepotea njia
Jyeah uzia na rupia kaelekea kibra ngamia bila ya dua
Huna miba samaki unajijua
Kwako haina shida upande wa pili kuliwa pia hey
Huna baraka thamani ya malapa ya choo cha nyumba ya kupanga
Mwenye haraka kutoa sadaka ya roho jeneza juu ya sanda
Wanakuita seremala sababu unalala kwa kila kitanda
Hiyo biashara Duppy nipe mizuka ya kinanda
Aah Toa mkwanja na ugonge unavyotaka
Wanaisoma namba funguo nyingi kwenye kitasa
Na anasa tetega mitego na wananasa
Fasta nishakuvua label huna mitego rudia darasa
Kipofu wa ngono unapapasa
Barua ya promo na mate mengi kwa kila bahasha
Umeungua midomo mpaka vipisi unaviwasha
Najiuliza sasa ni kipi hasa nilichodata

Nilidhani Deddy one and only kumbe nilikosea
Kila unachotaka unapata bado unazingua
Lango la jiji we unapenda chapaa (chapa)
Lango la jiji we unapenda chapaa (chapa)
Lango la jiji we unapenda chapaa (chapa)
Bye bye hunifai

Upendo kwako patashika unawaka ka lighter
Majigambo na kero ndo zimefika
We ni kunguru bonge la mbinde kufugika
Unatosha basi wa kichwani amesanduka

Napenda chapaa
Napenda chapaa
Unapenda chapwa
Unapenda chapwa
Napenda chapaa
Unapenda chapwa
Aii uuuhoo
Deddy ainadia
Na Stamina
Duppy

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI