MISTARI YA WIMBO HUU

Ladies and gentlemen

Mdogo mdogo ila kasi kama mbogo
Mi na dogo kama uso na kichogo
No mkorogo namba chafu soma logo
Spidi kali breki ya kwanza mpaka Togo
Mara mbili nikishusha kama gogo duuubwa
Mbio ndo nakamata kijiti
Physically mentally fit
Huu ndo namba moja kwenye list
Mbele kifuani kama njiti
Nakukill nafukia ka maiti
Yeah like father like son
Like Moon and Sun
Like war black lord
Chidi Benz The Return
Like fire like burn
Like mi kama fan
Like remix mchezo kwisha hapa yaani done

Done did
Na-come hivi na-run city
Ile kiBad Boy dizaini ya Biggie na Sean Diddy
Vyumba vimejaa wachumba
Vinega ni kazi ya wakubwa
So hakuna teenager
Mapendo daima ile kikatoliki
Mapenzi pesa sina kitu je ntapendwa kwa kipato kipi
He-he-he we unachekesha
Mi sio saizi yako boy ntakupwelepweta
Eh like father like son
You like others and I’m like non-think-twice fan
Kila nikispit huwa ni nice jam
Rap ya kuchana mpaka diaphragm bye son

Like father like son
Kama baba kama mtoto
Sijui utamgusa nani na wote wanawasha moto
Like father like son
Piga simu zima moto
Waambie beat inaungua mistari inaleta joto
Like father like son
Like father like son
Like father like son
Kama baba kama mtoto
Like father like son
Like father like son
Like father like son
Kama baba kama mtoto

Mungu hukumbukwa upesi kwenye shida bro
Hakuna mwizi wa kinyesi na wanalinda choo
Hawawezi shinda labda watapinda koo
Wananiita boy mimi kwenye ujinga poo
Kaa na mdosi utaona kama mkosi
Muda hauendi utasema ndo ile saa ya msosi
Sina chozi bosi of course ni hustler
‘Coz ni ratha
Kila picha kali hata nisipoweka pozi haswa
Leta cash nispit we’re the best in this
Wana-hate kichizi mademu zao wakikutana nami wananiita ‘Soonga’ (Naam)
Tunaweza piga selfie please

Record interview upate tuition ya hizi styles
Call me Zeus kwenye kitchen nahit the drum
Mi ni basi mi ni kazi
Mi sifai hivi why mi si-claim hizi lines with my son
when we vibe
Wanatufata fata fata ila wanatuogopa
Ondoka wanagwaya tunavyoondoka
Konga Songa ehee
Baba alishatoka ‘paka nimesota
So unaweza warm up
Hii ndo big teamz
In the mainstream with the big dreams
They respect it like the victims
We street kings
Did in real big thingz

Like father like son
Kama baba kama mtoto
Sijui utamgusa nani na wote wanawasha moto
Like father like son
Piga simu zima moto
Waambie beat inaungua mistari inaleta joto
Like father like son
Like father like son
Like father like son
Kama baba kama mtoto
Like father like son
Like father like son
Like father like son
Kama baba kama mtoto

Tungo safi na sio WCB
Nakohoa panchi utadhani na Hip Hop TB (koh koh)
Tafta chaki njoo uchafue CV
Weupe hawanitaki mi ndo Cheusi Dawa TV
Nikicheza hata gizani napiga bao
Mr Mayweather huwezi meza dozi ya Pacquiao
Kila jambo linalipa napanda pipa
Naacha sifa strika mbele ya goalkeeper
UH Cheza salama hizi zama za ibilisi
Mi ndo rapper wa gharama kwenye mziki wa bei rahisi
Ewe mamba muoga usifate msafara wa kenge
Hii track msiba wa shoga hauna sanda una kitenge

Naposamehea walonikosea haimaanishi ntawasahau
Ntawadharau ikitokea wakapotea kwa ubishi wao
Ikiwa kuishi kwao bila kusifiwa haifit kwao
Basi masnitch wao watakabidhiwa stitches zao
I go hard sio mikwara ka Gosby
Sirap kifala au kilingala sio Nyoshi
Au diblo dibala ka sigara mi moshi
Kankara ya Wara Wara haitoshi
Hii style ka kipofu mwenye pistol
Ni hatari akikoki jua ni kifo
Hakukosi ulipo siichoki na Hip Hop
Siitosi miko sifosi ujiko
Bosi malipo hautoki mshiko
Eeeheee

Chuki alekufunza nani
Hauzaliwi nayo unajikuta nayo ukubwani
Like father like son
Like father like son
Like father like son
Kama baba kama mtoto
Like father like son
Like father like son
Like father like son
Kama baba kama mtoto
Chuki alekufunza nani
Hauzaliwi nayo unaikuta nayo ukubwani

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI