MISTARI YA WIMBO HUU

It’s beautiful day
Asalaam aleikhum Tanzania

Nimeshatikisa nyavu mimi ndo MVP
Wakakimbia depo kwa polisi wa CCP
Niliwapigisha kuruta kwata la JKT
Nna kipaji mimi kushinda cha THT
Nawapangisha foleni kama bank ya NMB
Mimi nimesoma PCM sio PCB
So hata tufungwe mimi ni Arsenal sio Man U
Kibonde we ni member wa loan board au TCU
Nchi imeuzwa vigogo wanapita ATM
Tuwakemee mafisadi wote wa CCM
Kuvua gamba haiwasafishi mbele ya CUF
Chadema mwone Makamba JK kwa TFF
Sihitaji dancer wala mapanga yale ya TMK
Show zangu sio longo longo zile za Y2K
Na sio bandia kama lile kontena la BOT
Situkuzi kilichofake kama TOT
Mimi ndio Roma ntasimama kama KKT
Asante Bongo Makejoo na Mongo TBT
Mistari yangu mitamu kama miwa ya TPC
Na kwa hizi flow mamc mtalazwa KCMC

Kodi ya walalahoi pombe ya TRA
Miili yao ndio biashara ndani ya BBA
Fataki anatoa mkopo ndani ya TIA
Mimba hazina uhakika mpaka DNA
Mhaya ishike elimu
Msambaa auze matunda
Mpemba avue samaki
Mnyakyusa avune mpunga
Aah ah yah
Rock City mikono juu yeah
Mbeya City mikono juu

Mwambieni hatukuogopa tabiri za shekhe Yahya
Mahuti yangetufika bila kumpinga Jakaya
Sisaliti sirudishi kadi ya chama ka Nakaaya
Bado hainingii akilini hukumu ya babu Seya
Wagonjwa wanakufa mapokezi
Dokta anakunywa Value
Wazazi wanakufa labour wengine ICU
Wagonjwa wanakufa mapokezi
Dokta anakunywa value
Wazazi wanakufa labour wengine ICU
Waambieni mi mzalendo na hii ndo mbiu ya mgambo
Tanesco wakizima umeme hupitisha mzigo wa magendo
Harakati za dokta Ricky katika kuinua michezo
Mama Terry wamemsaliti mwasiti wamempa tangazo
Lady pepeta hawavai msema kweli Samunge
Mipira Hawaitumii eti kwa babu kuna kikombe
Mafuta wanapandisha bei kisa wanamiliki sheli
Wachina wanawapa tenda si tunanyimwa vibali
Gongo La Mboto wanalia misaada wamewatapeli
Bandugu bwaga manyanga ayaokote Magufuli
Pesa za ujenzi wa shule kala na mkewe headmaster
Thamani ya mabango ya kampeni somesha watoto Veta
Wanajiuliza dokta Slaa ni wapi anapata data
Hatakama nimevaa mlegezo ikulu napiga chata

Ikulu imejaa vibaka Manzese wanawakamata
Makahaba wanaongezeka boom linapokata
Wanauziana kwa minada mali za serikalini
Mhasibu anacheki porno si tumepanga foleni
Mmakonde chonga vinyago
Muha avue dagaa
Mmasai alinde geti
Mnyamwezi arine asali
Aah ah yeah
A city mikono juu yeah
Yeah Iringa mikono juu

Ma-emcee wanapata stress Roma akitua Ubungo
Tanga niliwafunga tatu nawafunga tano hapa Bongo
Wanafuga rasta ili wapate mademu wa kizungu
We mchaga kauze mitumba muziki ushakufunga pingu
Mistari yako myeusi it’s okay naipaka carolite
Katiba sio msaafu my people need copyright
Vuta pumzi ya baba ila kwa pua ya kitusi
Na siachi kupiga goti mbele ya Altare kasisi
Imamu akizini mjengoni usiukimbie msikiti
Padri akilala na sista aibadilishi ukatoliki
Hata gangster hulegeza macho (WHAT) ukimpa cotton buds
Mnakamata mateja wakati nyi ndo mnauza drugs
Ili ujue fegi imewaka lazima upige tafu
We baba usimtume mtoto aiwashe utamuua mapafu
Popote umuonapo ng’ombe jua hapakosi mmasai
Na Tongwe ndo ngome kongwe Zanzibar msinitoe nishai
Ndoto zangu kitambo ilikua nije kuwa padri
Zikayeyuka nilipopuliziwa moshi wa weed
Naenda church naamka tena nasali
Napopote utakaponiona shingoni nimevaa rozali
Hip hop ni conscious sio usharobaro kubeba nondo
Me natafuta pesa ya kula we unamcheki tu Alejandro
Unadhani utaandika nini kama sio hadithi za Konongo
Mi jamii inanihitaji kamuone babu wa Loliondo

Magazeti yanauza kwa skendo za wasanii
Machinga wanauza copy COSOTA wamekula deal
Shabiki anaburn nyimbo na show anaingia free
Underground usile ada urekodi ongeza bidii
Mzaramo acheze vanga
Mkurya apige kwata
Mdigo atungue nazi
Msukuma achunge ng’ombe

Aah you know Tanga is mine
Yeah Tanga mikono juu

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI