MISTARI YA WIMBO HUU

Mbele yako (mbele yako)
Nyuma yangu (nyuma yangu mie)
Usinichukie ewe ndugu yangu
Mbele yako (mbele yako)
Nyuma yangu (nyuma yangu mie)
Usinichukie ndugu yangu

Mbele yako nyuma yangu, twende kamanda wangu
Usiogope tuko na Mungu pekee, mwenye ulimwengu
Yoyote aliyeko hai simuhofii zaidi ya Jah anayenidai pumzi hii
Niko kama zamani, nimpinga shetani najiamini
Najua nifanye nini napokuwa majaribuni
Naomba dua, nasali na kufunga wachawi nawatambua
Nawaumbua, kwa maombi nawatenga hata kabla hawajaniua
Nawatimua, naenda kwa ndugu zangu wanaonipenda
Naowapenda kama navompenda Mungu
Maana nampenda Mungu kuliko mwanangu Tunda
Kuliko mama Tunda
Japo ni mwenzi wangu miaka rudi miaka nenda
Simtaji makusudi kwa vile anaweza kwenda
Tena anaweza kwenda wakati bado nampenda
Akaniacha peke yangu
Ama inawezekana akaniacha mi na mwanangu
Si unaelewa binadamu, ndo maana wenye ufahamu
Walisema mapenzi sumu
Yapo yenye utamu kama ya Eva na Adam
Lakini matokeo yake ndo hivyo yametuhukumu wanadamu

Mbele yako (ee ah)
Nyuma yangu (mbele yangu mie)
Usinichukie ndugu yangu (ndugu yangu eh)
Mbele yako (mbele yako)
Nyuma yangu (nyuma yangu mie)
Usinichukie ndugu yangu

Eh Mungu, Mungu wangu
Muone huyu mbona ana chuki kwangu
Japo hakiwezi kuja kwangu (never ever)
Mbele yako nyuma yangu (milele na milele)
Ukiangalia mabaya yangu (machache sana)
Lazima utaona na mazuri yangu (kibao, kibao hayahesabiki)
Bila kuongea inakuwa ngumu (hataki kusema ukweli)
Ngumu uh, sifa kwangu
Sielewi kisa nini, unaleta chuki na mimi
Tukikutana njiani (eti!)
Unakunja kisirani
Ulishazipanga ngumi (barabarani)
Kutaka pigana na mimi (haiwezekani)
Nikasema sipigani (never!)
Usela wa kizamani
Vipi unichukie, waomba mungu wako anifungie
Ridhiki yangu isinifikie
Au umeambiwa mwanga wako mie
Ikivuma sana ngoma hupasuka
Subiri mwisho wangu utafika
Chuki fitina utasumbuka

Mbele yako (mbele yako)
Nyuma yangu
Usinichukie ndugu yangu (usinichukie)
Mbele yako (mbele yako)
Nyuma yangu (nyuma yangu mie)
Usinichukie ndugu yangu

Kama zamani 20 na Sulemani
Wanaongea na kuongea, si bado tunaendelea
Kujizolea heshima sifa kibao
Ukipima mimi na wao utanielewa nachosema
Kwamba hata kama tembo akikonda hawezi kuwa kama ndama
Kazi ndo kwanza naanza
Kutokomeza na-rap na kukonyeza
Wanatongoza kila mkoa na mademu
Usiku mnene pombe nyingi, hivi unakumbuka condom
Oh! Okay kijana mdogo sisemi usiwe na demu
Lakini usiipe kisogo sheria mama ya hili gemu
Ukiacha ndumu, una uwezo kuandika rhyme kwenda gym
Trakindo kuonyesha ugumu
Bado una mambo mengi ya kujifunza kwenye game
Ili udumu, unahitaji kuwa na nidhamu ya kudumu
Sio ya kumzuga mwalimu, utajihukumu
Niamini baba ake Tunda
Natenda wema nakwenda, singoji asante ya punda
Ndo maana bado napanda
Na sitarajii kustaafu kwani mziki sio kandanda
Watu bado wanapenda, mchana usiku wananiuliza
“Kazi mpya lini kamanda   ”

Mbele yako (oo ah)
Nyuma yangu (nyuma yangu mie)
Usinichukie ndugu yangu (ndugu yangu)
Mbele yako (oo ah)
Nyuma yangu (nyuma yangu mimi)
Usinichukie ndugu yangu

Mbele yako nyuma yangu sio, au vipi
Imeshakuwa ya pili, toka kwa Sulemani wa pili
Aliyetunga Darubini Kali
A.K.A Simba zee kubwa na meno makali
Mkali wa mashairi
Mwenye jina lafanana na la mwana yule mtunga Zaburi
Wa pili kwa akili, japo bado sio tajiri
Mziki Bongo shubiri
Sio asali kama we unavyofikiri
Hata mkuu wa serikali analielewa jambo hili
Na amesema tusijali lazima atatupa dili
Ndo hivyo tunasubiri, au vipi
Mbele yako, nyuma yangu au sio
Salute sana, pamoja sana
Sambamba makini, Selemani Msine
Ai, woi
Ai, hahaha

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI