MISTARI YA WIMBO HUU

Nimeamini apangalo mola hawezi pangua yeye ndiye anayejua
Laiti ningejua jinsi alivyokuwa nisingejisumbua kumchukua
Mbaya sitaki
Twende dhihaki
We si rafiki
Mbaya sitaki
Nasema sitaki
Sitaki yuhaki mnafiki
Rafiki gani mdananda

Anapenda ku-bang hana kazi huyu jamaa
Na mastaa kadhaa wenye jina ndani ya Dar
Si nikajaa mi mzawa wa Dar na nikaachwa kwenye mataa
Nashangaa namba zake nimezidiwa mang’aa mashaka alikuwa kando
Nilihisi mchizi Bonge la mwana ah kumbe mgambo
Vitani hawezi kushika zana ah kweli kufa kufaana
Nimeamini ya leo sio ya jana (kweli ya leo sio ya jana)
Vizuri kufa na ujana ila life ya dunia ni tamu sana
Hizo sekunde na dakika bora zingerudi nyuma
Niwe bonge la bitozi hata salamu ningeuchuna
Mbio zimegonga ukuta kusanuka kishanuka
Na matuta nimeruka nimeanguka siwezi tena nyanyuka
Hata hata Shabaha alinitonya wewe ni rafiki bar
Nikapuuza kwa kujua na mzawa wa kitaa
Ghetto la Dar Stamina pia nikalitaa nilihisi kama nabanwa
Si ni wewe nilikulea ukiumia na-feel pain
Utetezi juu yako kama jeshi la UN
Ulidaiwa sikusita kukulipia madeni
Leo iweje uniingize mkengeni

Nimeamini apangalo mola hawezi pangua yeye ndiye anayejua
Laiti ningejua jinsi alivyokuwa nisingejisumbua kumchukua
Mbaya sitaki
Twende dhihaki
We si rafiki
Mbaya sitaki
Nasema sitaki
Sitaki yuhaki mnafiki
Rafiki gani mdananda

Nilikuwa ndani ya ghetto na-settle mipango ya kesho
Mara ring ring kucheki alikuwa mwana
Story ilikuwa hivi nanukuu michapo
‘Mwanangu sio siri una zali la mentali
Kuna binti mtaa wa pili anadai anakukubali
Anasema nyimbo zako unajua panga mistari
Tajiri hatari we kaa tuchume mali
Isitoshe ana figure matata hana dosari
Hata leo tukienda atakuhonga hata gari’
Kifupi sijajivunga na pozi zilikimbia
Urofa nilionao mnyamwezi nikajitupia
Pependo ulikuwa faster kama goli la feste
Tuliishi kwenye bungalow sio nyumba za gesti
Shida nilizishinda hata kwa Manji navimba
Kumbe nimepewa goma limepiku sindimba
Yule dada mwathirika nimetumika bila kinga
Na mchizi alishajua ninapotimba nachinjwa

Nimeamini apangalo mola hawezi pangua yeye ndiye anayejua
Laiti ningejua jinsi alivyokuwa nisingejisumbua kumchukua
Mbaya sitaki
Twende dhihaki
We si rafiki
Mbaya sitaki
Nasema sitaki
Sitaki yuhaki mnafiki
Rafiki gani mdananda

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI