MISTARI YA WIMBO HUU

Yeah
You know what Tiddy
One Love FX again man
It’s Moro town in the house
Shorwebwenzi on this one

Peleka kitanda batani ka unapenda ukeshe baa
Sista duu muda hausimami hata uivulie nguo saa
Ishi kiushujaa kama umepanga kambi ya jeshi
Kati ya maarufu na staa maarufu anaongoza kwa deshi
Ewe raisi wa wanyama fanya sensa usisahau
Mfuasi aliyesaliti chama huku mjini bonge la nyau
Tunza Bible sio hirizi ufalme wa mbingu hauna fensi
Ndo maana akifaga mzinzi mazishi hatufanyi gesti
Chagua kilicho best kati ya copy na ku-paste
Je yule aliyefeli maisha class alifeli test
Hakuna demu anaejiuza hiko ndo nikijuacho
Nachojua anakodisha unatumia huondoki nacho
Bitozi msaka mchumba usi-force unapotemwa
Piga goti kwa Muumba ikibidi akuumbe tena
Mguu moja pande mwingine urudishe sawa
Hii ndo ishara ya kiafande ya kuweka mambo sawa

Naamini ya nyuma ulikosea rudi
Weka mambo sawa na Plan B
Unaweza fanya bora zaidi muda bado
Mguu pande (moja)
Mguu sawa (moja)
Nyuma geuka (moja mbili tatu moja)
Mguu pande (moja)
Mguu sawa (moja)
Nyuma geuka (moja mbili tatu moja)
Mguu pande
Mguu sawa
Nyuma geuka

Yoh
Mjini wanyama kibao cha ajabu wanakula unga
Mawazo ya vichwa vyao dingi afe warithi nyumba hee
Ewe kengeza chunga usimcheke chongo
Cha msingi muombe Ebenezer akupe vision ya michongo
Saka chaka kila sehemu maana pesa ina machale
Nyie mnaowinda mademu hivi mna nyota ya mshale
Mnyamazie mshenzi ukimjibu tu anatuna
Hadi shoga nae ana mpenzi kweli mademu mna huruma
Mziki umejaa stress ambazo haziishagi kwa pombe
Mastaa wamewekeza Desi wanakufa hawana hata ng’ombe
Underground chonde chonde usiache shule kisa mziki
U-superstar una mabonde na miteremko ya dhiki
‘Yesu anarudi lini’ hilo swali ndo ujiulize
Sio ‘Stamina utaona lini’ ntajibu tu ‘niko busy’
Mguu moja pande mwingine urudishe sawa
Hii ndo ishara ya kiafande ya kuweka mambo sawa

Naamini ya nyuma ulikosea rudi
Weka mambo sawa na Plan B
Unaweza fanya bora zaidi muda bado
Mguu pande (moja)
Mguu sawa (moja)
Nyuma geuka (moja mbili tatu moja)
Mguu pande (moja)
Mguu sawa (moja)
Nyuma geuka (moja mbili tatu moja)
Mguu pande
Mguu sawa
Nyuma geuka

Yah
Usitupe mayai kiholela zalisha ili uache chata
Maisha baiskeli ya delela ukiinama chako unapata
Kumpa kibogoyo mnofu kisa nyama bei ya ghali
Sawa na kumteta kipofu huku kifikra anaona mbali
Hakuna zali la mentali kwenye sayari ya kupendwa
Mlevi mnywa safari je unajua unapokwenda
Acha mashauzi sista duu genge linalipa
Ujanja sio kwenda South au China ili ukawe stripper
Mapenzi ni kutendwa mtendaji jiamini
Sharo ukiona unapendwa ujue una nyota ya ukimwi
Ni sawa na uote usiku una-kiss na jini
Halafu uamke ujikute una lipstick kwenye ulimi
Unahitaji akili sio mashavu yenye dimples
Mwanaume jasiri hajichubui kisa ana pimples
Mguu moja pande mwingine urudishe sawa
Hii ndo ishara ya kiafande ya kuweka mambo sawa

Naamini ya nyuma ulikosea rudi
Weka mambo sawa na Plan B
Unaweza fanya bora zaidi muda bado
Mguu pande (moja)
Mguu sawa (moja)
Nyuma geuka (moja mbili tatu moja)
Mguu pande (moja)
Mguu sawa (moja)
Nyuma geuka (moja mbili tatu moja)
Mguu pande
Mguu sawa
Nyuma geuka

(My man Tiddy Hotter)

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI