MISTARI YA WIMBO HUU
Ni asubuhi ninaamka ninapiga mswaki
Kisha naenda kubaf kuweka mwili safi
Narudi ghetto nafungua kabati
Nachukua pamba bling bling kwa chati
Na t-shirt ya black
Na jeans ya khaki
Na chini nina simple white chata Nike
Kisha mzee najipulizia marashi
Pss
Nanukia safi
Niko na machizi wa Chambers Squad na Darky
Tunapiga simu Rich Coast wako wapi
Tunakutana mitaa ya Chaga Bite
Asubuhi tunapata zetu supu kwa chapati
Na mitungi ya kupotezea wakati
Ukitaka fegi mezani kuna pakti
Iwe Sport yani SM au Embassy
Hapa utakula raha mpaka mwenyewe utasema basi
Tunakamua mpaka ile mida ya lanchi
Tunaagiza ugali mkubwa na samaki
Makamuzi yanaendelea mpaka night
Watu wanaingia Graveyard kwanza kupata nyasi
Tunarudi kila mmoja anajisachi
Kiasi gani mfukoni kilichobaki
Kujicheki mi nna kama laki
Nikawaambia machizi kinachofuata mikasi
Mitungi
Blanti
Mikasi (ooh yeah)
Kama ukitaka kuvinjari nasi
Basi mfukoni mwako nawe uwe safi
Mitungi
Blanti
Mikasi
Kama ukitaka kuvinjari nasi
Basi mfukoni mwako nawe uwe safi
Kulewa tushalewa kilichobaki mikasi
Washikaji milupo tutapata wapi
(Milupo labda mitaa ya kati)
So tunaenda vipi kwa miguu au kwa basi
(Usiku huu bora tuchukue taxi)
Poa basi tusipoteze wakati
Kss kss naita taxi
Njoo utupeleke mitaa ya kati
Tukacheki midudu ya kupiga mikasi
Tuelewane kabisa itatucost shilingi ngapi
(Buku nne tu)
Aah wapi
Kwani hapa na pale ni umbali wa hatua ngapi
(Si mnacheki wenyewe mko wangapi)
Usimind sana babake tuko safi
Tuchangeni tusipoteze wakati
Ludi eh kwani we una shilingi ngapi
(Buku tano)
Venture
(Bati)
Sasa wewe una bati usiku huu unaenda wapi
Wakati hiyo bati hata soda tuu hupati
Bora uweke kesho unywee chai na chapati
Asie na kitu mi naona bora akabaki
Tusije mbele tukashikana mashati
Suka eh
Tuanzie Masaki
Mchizi kapiga simu yani kuna bonge la pati
Mitungi
Blanti
Mikasi (ooh yeah)
Kama ukitaka kuvinjari nasi
Basi mfukoni mwako nawe uwe safi
Mitungi
Blanti
Mikasi
Kama ukitaka kuvinjari nasi
Basi mfukoni mwako nawe uwe safi
Dereva funga breki tushafika kwenye pati
Eeh bwana eh kumbe bonge la pati
Cheki mademu kibao utadhani kichen pati
Duh!
Cheki lile anti lililovaa skintight
Ee bwana eh liko safi
Sio mchezo babake unaweza ukahonga laki
Aah wapi
Mtu kama mi hanipati
Usawa wenyewe huu wa kulenga kwa manati
Haya basi tujichanganye katikati
Tukacheki mitungi na mademu wa mikasi
Oh yeah braza mwenye black unaitwa na yule anti
Yuko wapi
Yule aliyevaa suti ya kaki
Aunty vipi
Aah safi
Samahani kwa kukupotezea wakati
Nilikuwa naomba tuwe wote kwenye pati
Au unasemaje
(Mi naona safi)
Samahani wewe anti ambaye umevaa shati
Hivi unaitwa nani eh
Naitwa Bahati
Hivi Aunty nishawahi kukuona wapi?
Acha longolongo we sema una shilingi ngapi
Oya we vipi
Mpango wako vipi
Mbona mi mazee mpango wangu safi
Ishakuwa usiku twenzetu tukachukue taxi
(Aha)
Twenzetu tukapige mikasi
Mitungi
Blanti
Mikasi (ooh yeah)
Kama ukitaka kuvinjari nasi
Basi mfukoni mwako nawe uwe safi
Mitungi
Blanti
Mikasi
Kama ukitaka kuvinjari nasi
Basi mfukoni mwako nawe uwe safi
Yeah yeah
Yeah yeah
East Zoo yo
Holler
Bongo Records
Ngwair
Ee bwana eh
Niko around mazee
No comments yet