MISTARI YA WIMBO HUU

Mateso unayonipa mwilini
Ni vigumu we kuyatambua usoni
Umeshanichoma mkuki moyoni
Siwezi tena kuishi duniani na wewe
Nionyeshe huruma yako we mama (we mama)
Nionyeshe huruma yako we mama (we mama)
Nionyeshe huruma yako we mama (we mama)
Kabla mimi sijafa kiama

Aah! Kabla kifo cha baba nilipata nilichotaka
Na toka alipoanguka sioni hata pa kushika
Dingi alivyonipenda nashindwa hata kueleza
Ndugu zangu walinuna walisema ananidekeza
Ndo maana alipokufa wakapanga kuniangamiza
Visa vingi wanafanya ila mimi namuachia Mungu
Mkombozi uliye juu, na muumba nchi na mbingu
Kama kweli unayaona matendo ya walimwengu
Naamini utasimama na utalinda maisha yangu
Maana siko salama na kisa ni urithi wangu
Ndugu wameniandama waipoteze roho yangu
Nami sina pa kwenda, na sina mtetezi wangu
Mama alishakimbia na akaniacha peke yangu
Nateseka kivyangu, mchana jua ni langu
Usiku mvua ni yangu
Oh!

Mateso unayonipa mwilini
Ni vigumu we kuyatambua usoni
Umeshanichoma mkuki moyoni
Siwezi tena kuishi duniani na wewe
Nionyeshe huruma yako we mama (we mama)
Nionyeshe huruma yako we mama (we mama)
Nionyeshe huruma yako we mama (we mama)
Kabla mimi sijafa kiama

Sasa, baada ya kifo cha baba
Mama aliniacha pekee, kasonga mbele kivyake
Miaka mingi ikapita sikupata salamu zake
Kwenye vyombo vya habari nikatuma ujumbe wake
Tena kuna gazeti nilitoa hadi picha zake
Waugwana walioziona walisema yupo Kigoma
Na zaidi wakanieleza kuhusu maisha yuko njema
Nikaenda kumtazama
Nipate kuhakikisha kama alipo ni salama
Mnajua uchungu wa mama, eh?
Hasa mkipotezana kwa muda usiojulikana
Kwa bahati njema nikampata
Bahati mbaya ikafata, najuta yalionikuta
Ni vigumu kuamini lakini ukweli nitakufa
Mama alinikataa, kwanza sikumuelewa nikabaki namshangaa
Kisha nikamuuliza, vipi mama una kichaa?
Mwenyewe umenizaa, hivi sasa unanikataa!
Jibu alilorudisha sikuamini kwa masaa
Alisema sikujui na geti akafunga pah!
Shoga zake jirani wakanieleza kwa ufasaha
Kumbe kaolewa tena na amesema hajazaa
Hivyo angenikubali mumewe angemkataa
Mwili ulikosa nguvu nikabaki nimeduaa

Mateso unayonipa mwilini
Ni vigumu we kuyatambua usoni
Umeshanichoma mkuki moyoni
Siwezi tena kuishi duniani na wewe
Nionyeshe huruma yako we mama (we mama)
Nionyeshe huruma yako we mama (we mama)
Nionyeshe huruma yako we mama (we mama)
Kabla mimi sijafa kiama

Kweli nilishangaa
Mama ‘angu alionizaa kuniacha kwenye mataa
Takribani nusu saa sikuongea kama bubu
Watu walinizunguka, nikainama chini kwa aibu
Ntaishi vipi ugenini, akilini sikuwa na jibu
Kule sikuwa na ndugu, nkaishi maisha ya tabu
Sometimes ilinibidi nilale nje kama bawabu
Mbu, baridi kali, kwa kweli nilipata tabu
Maisha kwa kiumbe mimi yalionekana kama adhabu
Na kama unavyoelewa wenye pesa wengi waarabu
Wapo wenye ustaarabu, ila wengine hawana adabu
Nilipoomba msaada walitaka kwanza taarabu
Washenzi, hamna adabu
Ndivyo mimi nilivyo wajibu
Dhiki ukiendekeza haki ya Mungu watakuharibu
Hilo nililelewa nikaliweka kumbukumbu
Nilipokosa chakula ilibidi nilale njaa
Nikikosa pa kulala nazuga kwenye mitaa
Maisha kifo mkononi, kifupi mi niliishi kama mtoto wa mtaani
Ndo maana naona mbali, naona mbali
Kwa darubini kali!

Mateso unayonipa mwilini
Ni vigumu we kuyatambua usoni
Umeshanichoma mkuki moyoni
Siwezi tena kuishi duniani na wewe
Nionyeshe huruma yako we mama (we mama)
Nionyeshe huruma yako we mama (we mama)
Nionyeshe huruma yako we mama (we mama)
Kabla mimi sijafa kiama

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI