MISTARI YA WIMBO HUU

Hakuna S bila O, L bila O
Mwingine aitwa Thang bila Solo
Shupavu, awajibike kama Apollo
J, Afande, ni ukuta wapi chochoro
Hakuna S bila O, L bila O
Mwingine aitwa Thang bila Solo
Shupavu, awajibike kama Apollo
J, Afande, ni ukuta wapi chochoro
Hiyo naghai, ni mtazamo wa fani
Ile dhana ni uhuni wameleta wa katuni
Kuna ku-rap na kubwata
Marepper na ma-rapper
Katuni, tungo tata
Wapi ulipo we kaa
Unakuwa mtuma ili upewe promo kuuza
Au kama ni binti ukalale kwa producer
Ma-promoter wanauma tu, na hawajui na kupuliza
Na siku wakipuliza jua kidonda kishaoza
Natamani kuwa huru mnyonyaji asinidhuru
Wanaitwa ma-emcee hawajui mitindo huru
Huu mtazamo wangu naona vingi vioja
Yaani watangazaji sasa ndo ma-manager
Vidato sita nilivyopitia ndivyo vinavyonisaidia
Mbunifu ukizingatia, hata wakinibania
Ni kipaji tu, ni mtazamo tu
Msikasirike washikaji haya mawazo tu

Ni mtazamo zamo emcee usiogope kivuli
Bora ukemee mabaya na usifie mazuri
Ni mtazamo zamo emcee usikwepe umande
Okoa sanaa ya Bongo ili uchumi upande
Ni mtazamo zamo emcee usiogope kivuli
Bora ukemee mabaya na usifie mazuri
Ni mtazamo zamo emcee usikwepe umande
Okoa sanaa ya Bongo ili uchumi upande
Kwi kwi, Ulamaa, Professor Jay, Afande

Ni mtazamo rap inakuwa ni mikingano
Sasa watoto wadogo wanajiita watu wa makamo
Wanakwenda hatua mbili, wanarudi kumi na kujipongeza
Bila kuzingatia hatua nane walizopoteza
Hao ni mafukara wa akili zao na uwezo wao
Wasiotambua nini na nini ni hatima zao
Magwiji vichwa chini nadhani wanatunga sheria
Lakini sheria msumeno isije ikawarudia
Yes, ma-underground wanafanya rap inang’ara
Lazima muwe vinara imara kwenye msafara
Rap na mazingaombwe abadani, haviendani
Msitegemee tawilee iwaokoe katika fani
Ni vyema ukafikiri kabla ya kufanya maamuzi
Tazama mbele usije ukanywa chai kwa mluzi
Naamini askari shupavu lazima upitie depo
Vinginevyo ndugu yangu utakuwa unapaka rangi upepo
Kama unapata moja kwanini usipate na mia
Hiyo inawezekana kwa wote mlio na nia
Sioni sababu za msingi kuomba kwenye mitaa
Kama una kipaji iweje ufe na njaa

Ni mtazamo zamo emcee usiogope kivuli
Bora ukemee mabaya na usifie mazuri
Ni mtazamo zamo emcee usikwepe umande
Okoa sanaa ya Bongo ili uchumi upande
Ni mtazamo zamo emcee usiogope kivuli
Bora ukemee mabaya na usifie mazuri
Ni mtazamo zamo emcee usikwepe umande
Okoa sanaa ya Bongo ili uchumi upande
Kwi kwi, Ulamaa, Professor Jay, Afande

Asante Professor Jay
Majani na Ulamaa mmegusa n’napopataka
Nami kwenye mtazamo nina jambo nataka kuweka
Maana kila kukicha emcees wanaongezeka
Nasema very nice, yes rap kama dhehebu
Emcees kama wafuasi
Wingi wa wasanii unaonesha ni dini safi
Yaani imekubalika, waumini tuko wengi
Lakini bado nashaka
Sijapata uhakika, wote tumesadiki
Ama wengine ni fake mmetumwa kama mamluki
Maanake hamna maana
Mna-rap mnadi rap, mistari imekosa vina
Yenye vina haina maana
Na kila mnapokaa mnapenda kusengenyana
Mnapenda kutetana na mnapenda kurumbana
Mimi naogopa sana
Kwa jinsi navyoelewa mwishoni mtatukanana
Ama inawezekana mwishoni mkaja chinjana
Na wote tunao-rap tuonekane hatuna maana
Wapi ilipo Taarab
Ilikuja kwa kishindo, hata wagumu walishausudu
Kwa ajili ya marumbano mwishoni ikafa kibudu
Shabiki piga simu, changia mawazo yako
Nani tutamlaumu, kama rap ita-cease kwa kuendekeza upuuzi
Nani tumchune ngozi, producer aliyerekodi
Ama labda DJ anaepiga kwenye kipindi
Wengi wanapenda rap, ajabu rap haiwapendi
Waungwana wanaiacha, wapumbavu hawaambiliki
Hivi kwani lazima tuwe wote wanamuziki
Mi nadhani ingetosha wengine mbaki ushabiki
Huu ni wangu mtazamo masela msijenge chuki
Hata na Majani, yoh

Ni mtazamo zamo emcee usiogope kivuli
Bora ukemee mabaya na usifie mazuri
Ni mtazamo zamo emcee usikwepe umande
Okoa sanaa ya Bongo ili uchumi upande
Ni mtazamo zamo emcee usiogope kivuli
Bora ukemee mabaya na usifie mazuri
Ni mtazamo zamo emcee usikwepe umande
Okoa sanaa ya Bongo ili uchumi upande
Kwi kwi, Ulamaa, Professor Jay, Afande

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI