MISTARI YA WIMBO HUU

Ukimya ni busara
Mwendo mdundo ndo yangu sera
Jah yu nami
Nidhamu nipe hela
Sijawatupa my fans,najuwa mpo nami
Let me say
Mwendo mdundo (Mwendo mdundo)
Mwendo mdundo (Mwendo mdundo)
Mwendo mdundo, jah yu nami

I say ana-ana, ana-ana dooh
it’s your boy from Sinza,you alredy know
Nachanika tu mistari kwenye microphone
Nina pumzi ya kutosha kwenye hii marathon
Kitambo sana tangu uliponiskia
Young black and gifted,siwezi potea njia
Shut up and listen,nawapa watu dawa
Kwani kuwa MC ni kazi ya kuweka watu sawa
Kurudi chuo walidhani nimeshasanda game
Ama proving them wrong,kwa hii mistari wamesha-confirm
Nilikuwepo, nipo na nitazidi kuwepo
Nawakilisha mitaa na maisha ya gheto
I am Hip Hop, na ujumbe unafika
Hili ndo’ lengo kuu na siyo bora kusikika
I think deeper ndo’ mana KINA KIREFU
Na bado huwezi nielewa ikiwa siyo mwerevu
(yeeeaaah) Waliniuliza, Mansu-Li mbona kimya
Hatukusikii redioni,vipi umeishiwa vina
Sikuwa na la kujibu hivyo nikanyamaza kimya
Ila muda ndo’ unaongea na hivi navunja ukimya

Ukimya ni busara
Mwendo mdundo ndo yangu sera
Jah yu nami
Nidhamu nipe hela
Sijawatupa my fans,najuwa mpo nami
Let me say
Mwendo mdundo (Mwendo mdundo)
Mwendo mdundo (Mwendo mdundo)
Mwendo mdundo, jah yu nami

Rest in peace Banza Stone, Sinza is on my shoulder
Na popote niendapo naibeba hata kama boda
Mjeshi anapokufa mwanajeshi anazaliwa
Na bado sauti inaskika mpaka kanda ya ziwa
Popote kambi, iwe nyumani ama ugenini
Ushindi nje na ndani,kwa sababu najiamini(najiamini)
Pancho Latino,mpe salamu Hermy B
Mwambie kwangu ni ndugu kama Dunga na Shakii(Dunga na Shakii)
Sijawahi kuwa na beef na CP Eti sababu ya beat,meeen am to real
Nafanya muziki wangu pasina beef na mtu
Ila napoongea ukweli wengine wanajishuku
Sipotezi muda,napiga vishada
Kama JCB na MOE,shout out kwa J-MURDER
Hatupotei, hatukosei
Tunakwenda tu likizo,tukirudi hatungojei
Mikono mfululu yani paa paa pah
Tangu oldskul, newskul rat-tat-taah
Mwendo mdundo, sijasanda nipo full (nipo full)
Halinipati dua la kuku nipo juu
You run this town,me na-run everywhere
Hakika Jah yu nami,you better stay clear

Ukimya ni busara
Mwendo mdundo ndo yangu sera
Jah yu nami
Nidhamu nipe hela
Sijawatupa my fans,najuwa mpo nami
Let me say
Mwendo mdundo (Mwendo mdundo)
Mwendo mdundo (Mwendo mdundo)
Mwendo mdundo, jah yu nami

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI