MISTARI YA WIMBO HUU

Hivi ni nini kilichokusibu
Message zangu huzijibu
Akili yangu unaiharibu unaiharibu unaiharibu
Si ka zamani hatupo karibu
Fanya kweli au wanjaribu
Kila nipitapo nasikia aibu
Hebu punguza hizo zako ghadhabu
Ka unalo swali mi ntajibu
Nishagusi anaejua atakwambia
Ona sasa mtaani wanaongea
Haiwezekani kwanini nikakosea
Sina budi kukidhi mi niliendekeza
Sasa naomba nafasi kwako kuiendeleza
Basi mpenzi punguza manuno
Naomba uelewe hili langu somo
Bahati mbaya mpenzi usianze mgomo
Penzi lako kwangu lisifike kikomo
Tamaa yangu unajua nichosha
Akili yangu unazidi kuidatisha

Mpenzi naomba nafasi nyingine
Zaidi yako mimi sina tena mwingine
Mambo yangu mi sifanyi (mambo yangu mi sifanyi)
Nakuwaza wewe (nakuwaza waza wee)
Mwili unatweta naweweseka nateseka

Nielezee
Nifanye nini unisamehe
Nielezee
Nifanye nini unisamehe
Nielezee
Nifanye nini unisamehe

Hey hey
Ama nipige magoti nikulilie
Sema basi kitu gani nikufanyie
Au nini mpenzi wangu nikununulie
(Ili mradi tu unirudie)
Kumbuka ahadi tulizopeana kitandani
Na mambo mengi tuliofanya gizani
Leo hii hayana thamani
Kama kweli uliyatilia maanani
Mpenzi wangu usijeniacha hadharani
Kukuvumilia kote dharau
Wema wangu wote umeusahau
Hautambui wala hujui nana nau nanau
Hutambui wala hujui nana nau nanau
Ni vigumu kiasi gani kutafuta mwingine
Hey hey he-he he-hey hey

Mpenzi naomba nafasi nyingine
Zaidi yako mimi sina tena mwingine
Mambo yangu mi sifanyi (mambo yangu mi sifanyi)
Nakuwaza wewe (nakuwaza waza wee)
Mwili unatweta naweweseka nateseka

Kukoseana kwenye mapenzi si ajabu si kitu cha ajabu

Kama kweli waelewa sasa ya nini unipe tabu unipe tabu hey

Wacha kunisononesha mpenzi nipe jawabu jawabu

Au ndo umeamua kunitafutia sababu sababu hey

Na nshajifunza sasa kutokana na makosa
Na nshajifunza sasa kutokana na makosa
Honey I’m sorry (I’m sorry I’m sorry)
Baby I’m sorry (I’m sorry I’m sorry)
Honey I’m sorry (I’m sorry I’m sorry)
Baby I’m sorry (I’m sorry I’m sorry)

Mpenzi naomba nafasi nyingine
Zaidi yako mimi sina tena mwingine
Mambo yangu mi sifanyi (mambo yangu mi sifanyi)
Nakuwaza wewe (nakuwaza waza wee)
Mwili unatweta naweweseka nateseka
Mpenzi naomba nafasi nyingine
Zaidi yako mimi sina tena mwingine
Mambo yangu mi sifanyi (mambo yangu mi sifanyi)
Nakuwaza wewe (nakuwaza waza wee)
Mwili unatweta naweweseka nateseka

Mpenzi naomba nafasi nyingine
Mambo yangu mi sifanyi nakuwaza waza wee

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI