MISTARI YA WIMBO HUU

Nawakilisha
Ofisini na masela ndani ya ghetto
Nawakilisha
Kwa madingi, vijana mpaka watoto
Nawakilisha
Kenya, Uganda na Tanzania
Huu ni wosia, bila umoja hakuna njia
Nawakilisha
Ofisini na masela ndani ya ghetto
Nawakilisha
Kwa madingi, vijana mpaka watoto
Nawakilisha
Kenya, Uganda na Tanzania
Huu ni wosia, bila umoja hakuna njia

Hii ndio aridhi ya Mugabe, brother shoga huwezi kuishi
Nimefika rapper mbabe, kazi kwako rapper njiti
Tupa shuka andaa tanzia mazishi
Wananiita chief cooker maana napika hadi maandishi
Tangu nazaliwa nina mzuka wa mistari
So usistuke unapohadithiwa kwamba mimi rapper mkali
Kunywa sumu na maziwa, shusha tanzi juu ya dali
Uwe na uchungu wa kufiwa ka uliona kifo asali
Wa Pemba panda mtumbwi, wa Moro nipande basi
We hushangai Kigoma vumbi ila imetoa wasafi
Upeo niliopewa, umezidi hadi lenzi ya bundi
Bado wanaogopa kuongea kama wametema mkali wa kundi
Sistushwi, na nyinyi sanamu wa urembo
Hadi swala aliyetoka bush leo mjini anatishia matembo
Shujaa wa movie yenu leo anakufa kwenye trailer
Nahamisha vichwa vyenu sujudu ili uunge tela, ah
Sina ruzuku nina mtoto wa ma-punch
Hata nikifa kapuku sikosi buku kila lunch
Tozi nyoa duku, ingia booth uimbe cranckie
Utoe ngoma ya kikasuku yenye utundu wa ku-dance
Nilizaliwa mwanaume, sio ili nivae kaptura
Bali ni-fight kiume nyumbani waweze kula, ah
Unda tume uje unishushe power Mabula
Na nyota pakashume sidati na uzuri wa sura
Masoud Kipanya ‘nsie na shimo ya kujificha
Mi Sadam mwenye mwanya ndo maana sipigagi picha
Niite ticha, ili ukikosa nikupe mji
Ukinikuta navuta shisha utasema breakdown ya jiji
Nilikotoka mbali na nashukuru nilipo
Hata ninyimwe salary maisha yangu yatabaki simple
Walipo mi sipo, na nilipo hawapo pia
Vipi wanaremba mwandiko kwenye daftari la tanzia?!
Sitaki kitimoto, nataka kiti cha enzi
Funga ndoa na Asha Boko ka unahitaji ukubwa penzi
Mi ni mshenzi, tena mwenye tenzi tofauti
Nsie na hela benki, japo na akaunti ya wavuti
Sina uchawi hata chembe, nimemuacha Yesu ghetto
Sijatokea Milembe ila natema rhyme mental
Shaulin tempo, nachapa kila mdundo
Kinywa changu bado depo, karibu ewe fata-mkumbo
Salamu Goriati, Daudi nakuombea
Hata ukitaka mtu kati, mi mapigo ka San Deo
Leo ndio leo, zima TV washa video
Umuone emcee mwenye maarifa anaevuma kila leo, ah
Mjini mahaba karibu nikupe habari
Kitaani usawa unakaba gawa penzi kwa kamari
Mi amplifier, na-boost sauti isikike
Masoud sura mbaya ‘naependwa na watoto wa kike, eh!
Nimemaliza, heheh

Nawakilisha
Ofisini na masela ndani ya ghetto
Nawakilisha
Kwa madingi, vijana mpaka watoto
Nawakilisha
Kenya, Uganda na Tanzania
Huu ni wosia, bila umoja hakuna njia
Nawakilisha
Ofisini na masela ndani ya ghetto
Nawakilisha
Kwa madingi, vijana mpaka watoto
Nawakilisha
Kenya, Uganda na Tanzania
Huu ni wosia, bila umoja hakuna njia

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI