MISTARI YA WIMBO HUU
Kama mama anavyompenda mwana toka tumboni
Nami ndivyo nilikupenda tangu zamani
Moyo uliniuma pale ulipoweka donda
Nafsi ilisononeka huku ikisema
Moyo uliniuma pale uliponiongopea
Nafsi ilisononeka huku ikisema
Kamwe sitopenda maishani na dunia
Wewe ubaki peke yako na mimi kivyangu
Nia yangu nsikuwaze
Kwenye moyo wangu unitoke
Ili moyo upoe
Na donda la moyo lipone
Nia yangu si mbaya
Najinusuru mapema
Akijikwaa mmoja
Nami wa nyuma kujikinga
Nia yangu nsikuwaze
Kwenye moyo wangu unitoke
Ili moyo upoe
Na donda la moyo lipone
Nia yangu si mbaya
Najinusuru mapema
Akijikwaa mmoja
Nami wa nyuma kujikinga
Ulipokuja kuishi nami kama mwandani
Mwenye nzuri tabia, uzuri wa sura
Na burasa pia
Kukupenda nilijisumbua
Kumpenda asiopendeka
Moyo wangu naomba uachie upumue
Kukupenda nilijisumbua
Kumpenda asiopendeka
Moyo wangu naomba uachie upumue
Nia yangu nsikuwaze
Kwenye moyo wangu unitoke
Ili moyo upoe
Na donda la moyo lipone
Nia yangu si mbaya
Najinusuru mapema
Akijikwaa mmoja
Nami wa nyuma kujikinga
Nia yangu nsikuwaze
Kwenye moyo wangu unitoke
Ili moyo upoe
Na donda la moyo lipone
Nia yangu si mbaya
Najinusuru mapema
Akijikwaa mmoja
Nami wa nyuma kujikinga
Mmh
Nia yako unilize
Moyo wangu uutese daily
Kosa lako unanigeuzia mie
Nia yako unilize
Moyo wangu uutese daily
Kosa lako unanigeuzia mie
Nimekushtukia (oh hoo)
Unajiongopea wewe
Kosa lako unanigeuzia mie
Nimekushtukia (oh hoo)
Unajiongopea wewe
Kosa lako unanigeuzia mie
Nia yangu nsikuwaze
Kwenye moyo wangu unitoke
Ili moyo upoe
Na donda la moyo lipone
Nia yangu si mbaya
Najinusuru mapema
Akijikwaa mmoja
Nami wa nyuma kujikinga
No comments yet