MISTARI YA WIMBO HUU

Yeah
You know what Tiddy
One Love FX again man
It’s Moro Town in the house
Shorwebwenzi on this one

Mi tajiri wa mashairi siwezi zamia kwa mkaburu
Nikitaka msichana jasiri ntatuma mshenga kwa Lulu
Wanani-diss bure huku nalipwa napochana
Style zao sare za shule huyu na yule wanafanana
Eti Stamina sio Hip Hop hey I don’ give up
Shahidi shabiki kwenye hizi boom bap
Kila goma nalotupa wanahamaki hawafichi fire
Rap kwangu kama Sutra naifanya kwa kila style
Wana mistari mikali ila hawaandiki vitu special
Fake hawana zali vizungu zungu a k a Recho
Ndo maana namshangaaga emcee akiniita whack
Wakati shoo anazofanyaga hajawahi kulipwa hata laki eh
Leta pesa kwa pocket nitoe ma-vocal ya ki-rich
Mdomo wangu sio socket vipi wanataka ni- switch
Sh*t Leta unoko nitabaki namba moko
Nyie vuteni shisha Coco mi navuta mjengo Boko

Panga pangua utanikuta niko ndani
Ndani kwenye fani kwenye chart namba one
Sukuma usukani cheza na wapinzani
Uone kama ujapiga mbizi kwenye lami
Huu ni mziki me do it for the love
Nanyi mashabiki basi mnge-show love
Sisi bado kwenye top nanyi mnge-show love
Somebody show love
Show show show show show love
Show show show show show love

Daily namba moko bila nguvu za miujiza
Wapinzani hawana soko hawauziki hata kwenye giza
Sichongi kitanda ntalala tu siku akifa
Sina undugu na Mwampamba kivipi nibaki mwisho
Bora peke yake adili mamluki mtan’nyima mtonyo
Salamu muheshimiwa waziri rudisha mziki wa Sonyo
Shusha bendera ipepee nusu mlingoti
Hii bombasa ya masela usicheze huku umekunja goti
Aah Leta maringo tupo lindo la mateja
Rap imenipa bingo sio ngombingo kwa vinega
Toka chimbo nafanya bila manager
Na-hitisha mpaka jingle nini single za vibega
Relax it’s yo’ boy Shorwebwenzi
Lile shamba la vina lilopandwa mistari kwenzi
Sijiiti komando ikiwa Amza bado hajalala
Masharo wakina Alehandro amka tizi na hizi dala
Sikuja Dar kuliona jiji nimekuja kimaslai
So hakuna pengo la Fid kama jembe niko hai
Mi ni pombe ya mistari ninywe uamke na hangover
Emcee mkali mentali leo na-takeover

Panga pangua utanikuta niko ndani
Ndani kwenye fani kwenye chart namba one
Sukuma usukani cheza na wapinzani
Uone kama ujapiga mbizi kwenye lami
Huu ni mziki me do it for the love
Nanyi mashabiki basi mnge-show love
Sisi bado kwenye top nanyi mnge-show love
Somebody show love
Show show show show show love
Show show show show show love

Somebody show love
Somebody show love
Somebody show love
Somebody show love
Somebody show love

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI