MISTARI YA WIMBO HUU

S.O.N.G.A
Songa
Niko na Cjamoker
Mmh
Tuko chimbo

Baada ya mishe mishe na taabu
Nikaamua ni-cease counter nizizike ghadhabu
Ila cha ajabu (nini)
Nikapokea meseji mtu simjui
Eti ‘Hi baby wassup’
Kabla sijamjibu nikacheki picha WhatsApp
Nikaona sura ya mrembo aliyeumbika
Uzuri wake ka kajiumba mwenyewe
Nikapozi nikamwambia waiter leta chupa nilewe
Yeah Huku nikiwaza hii text
Ni kweli amekosea namba au ananitest
(Siamini) ila haina noma fresh
Nikamjibu ‘cool’ huku nikisikiliza ngoma za Ray C
Mtoto akataka atume picha
Ili nimkumbuke anadai muda mrefu umepita
Kiuhakika nikamjibu poa we tuma naimani zitafika

WhatsApp Facebook mpaka Insta (picha)
Badoo Telegram mpaka Twitter (picha)
Kila kona mazee nayopita
Nakutana na (picha)
Nakutana na (picha picha)
WhatsApp Facebook mpaka Insta (picha)
Badoo Telegram mpaka Twitter (picha)
Kila kona mazee nayopita
Nakutana na (picha)
Nakutana na (picha picha)

Macho yangu hayakuamini
Alivyotuma picha nikasema ni yeye au ndo camera 360
Kwanza ni mzuri hupandi dau maskini
Alivyo msafi ntatembea nae peku viatu vya nini
Mara katuma picha na kimini
Akaona haitoshi nyingine akapiga na bikini
Mtoto ana figure kuuliza ana miaka 20
Nikaahidi kuwa nae aache vibaka wa mjini
Akadai na picha zangu anazihitaji
Mi nikatuma nilizopiga kwenye magari ya washikaji
Nikajiongeza thamani ili asinione choka mbaya
Akanitema huku akisema ni mzugaji
Basi mazoea yakazidi
Tukapanga tuonane ili tujuane zaidi
Siku ya kuonana nikaulamba moka na suti
Ila nilivyomuona live tu mwana nikatoka nduki

WhatsApp Facebook mpaka Insta (picha)
Badoo Telegram mpaka Twitter (picha)
Kila kona mazee nayopita
Nakutana na (picha)
Nakutana na (picha picha)
WhatsApp Facebook mpaka Insta (picha)
Badoo Telegram mpaka Twitter (picha)
Kila kona mazee nayopita
Nakutana na (picha)
Nakutana na (picha picha)

Yeah mh
Kwanza ngoja
Nayosema ni kweli na sio kwamba vioja
Kumbe ni bibi ambae anajikongoja
Na hata akisimama figure yake ni kama moja
Mwenzenu sina hamu na picha
Kuanzia WhatsApp Facebook Instagram mpaka Twitter
Yaliyonikuta kiukweli inasikitisha
Nashindwa kujuta nabaki kutikisa kichwa
Picha

WhatsApp Facebook mpaka Insta (picha)
Badoo Telegram mpaka Twitter (picha)
Kila kona mazee nayopita
Nakutana na (picha)
Nakutana na (picha picha)
WhatsApp Facebook mpaka Insta (picha)
Badoo Telegram mpaka Twitter (picha)
Kila kona mazee nayopita
Nakutana na (picha)
Nakutana na (picha picha)
WhatsApp Facebook mpaka Insta (picha)
Badoo Telegram mpaka Twitter (picha)
Kila kona mazee nayopita
Nakutana na (picha)
Nakutana na (picha picha)
WhatsApp Facebook mpaka Insta (picha)
Badoo Telegram mpaka Twitter (picha)
Kila kona mazee nayopita
Nakutana na (picha)
Nakutana na (picha picha)

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI