MISTARI YA WIMBO HUU

Tukianzia uzuri tu
She got a gwan
Tabia heshima ndio duu
She got a gwan
Mpaka kwa masista duu yeah
Nabaki tu kusema uh
She got a gwan

Mara ya kwanza mi namuona
East Zoo Dodoma
Ghafla nakajihisi kama mtu mwenye homa
Kutoa salamu tu jibu lake ni noma
Sauti yake tu nkajihisi nimepona
Ndefu yake shingo mwendo wa maringo
Nilifurahi aliponiambia yuko single
Sio siri mtoto huyu ameumbika
Na kama akipita mbele ya watu kumi basi
Nane kati yao lazima watababaika
Hata hao wawili wivu tu umewashika
Kila saa kwa Ngwair ndo amefika
Nami naapa kamwe sintomuacha
Mi naimani atanizalia mapacha
Na hata kama bahati mbaya akiwa tasa
Mnajua sitoweza kumuacha
Na yote ni sababu tu
She got a gwan

Tukianzia uzuri tu
She got a gwan
Tabia heshima ndio duu
She got a gwan
Mpaka kwa masista duu yeah
Nabaki tu kusema uh
She got a gwan

Sitosahau mara ya kwanza ameniruhusu
Nimbusu nitomase zake chuchu
Naona fahari leo mpenzi uko na mimi
Na ninaahidi milele ntakuthamini
Sitojali ashatembea na wangapi
Kuwa nawe maishani naona bahati
Kila unapopita masela unawadatisha
Babaisha wanabaki macho juu juu
Wakuonapo maduu wanakasirika
Kunja ndita wanabenua midomo juu
Najua yote hiyo ni wivu tu
Washakuzushia mambo mengi tu
Ila wewe ndio my baby girl mmoja wa pekee
Siwezi kuwa na raha bila kuwa na wee
Na kosa naomba unisamehe
Nataka kuwa na wewe milele
Okay
You got a gwan

Tukianzia uzuri tu
She got a gwan
Tabia heshima ndio duu
She got a gwan
Mpaka kwa masista duu yeah
Nabaki tu kusema uh
She got a gwan

Nionyeshe ulichonacho ma
Nionyeshe zaidi ya nguo zako ulizovaa
Nionyeshe zaidi ya ngozi yako ya kung’aa
Nionyeshe kile ambacho kitanipa raha (hey hey hey)
Girl you got a gwan
You’re my number one
And nia yangu mi ni kuwa nawe maishani
Chochote unachotaka mi ntakupa weka imani
Na mi naahidi kamwe wala sitokuacha njiani

She got a gwan
(Yes I know)

Mama get busy twende kwenye dance floor
Unapokata kiuno matozi wanapagawa
Utasikia sauti zao wakisema yeah yeah yeah
Na atakae shobokea mi ntamtoa dunia
Na kuanzia leo ntakuwa natembea mi na gun (ooh)
Naona milupo imeanza kuntamani
Basi malizia kinywaji twende zetu nyumbani
Girl

Tukianzia uzuri tu
She got a gwan
Tabia heshima ndio duu
She got a gwan
Mpaka kwa masista duu yeah
Nabaki tu kusema uh
She got a gwan

She got a gwan
Girl you got a gwan
Uzuri kuwa na wewe sio siri naona furaha
You got a gwan
Girl you got a gwan
Oh baby wewe ndo my number one
Number one
Number one
You’re the one

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU