MISTARI YA WIMBO HUU

Mbeya City boy
Ray V Vanny boy
Hey yo Laizer Can you raise it a lil bit
But u never saw this am coming

Kama Zidane mpira upo gambani
Vile navyo wabana kama pochi ya dada kwapani
Na mwamini Mungu funga virago shetani
Joh-Makini akiwa mweusi Baraka tumwite nani
Kwene biti nateleza japo sijasoma nachana hadi Kiingereza
Good morning (how are you) men that’s simple
You do it for your own but I do it for my people
Nisha taabika wala sikusikika
Wakala washika sahani nikakosa niliyepika
Sasa mambo yamejipa kila kitu uwakika
Nanenepa Wasafi kupiga selfie na Tiffah

Wananiita Sugu (nani)
Wananiita Sugu (nani)
Sugu Sugu Sugu (Rayvanny Boy)
Wananiita Sugu (nani)
Wananiita Sugu (nani)
Sugu Sugu Sugu

Naitwa Rayvanny Boy Vee Vanny langu jina
Kinyago toka Mbeya sio toy la Kichina
Sijatoboa sikio sijui piko wala hina
Tattoo ya kazi gani ngozi tayari ilishazima
Visirani walio kesha kupiga pini
Hawaamini nikipita wanaomba picha na mimi
Zamani mademu walinipiga chini
Saizi wananisumbua wao Ray jibu langu lini
Heshima kwa watabiri waliosema nitafeli
Wakaniita bajaji sitopita kwenye reli
Sasa ni Wasafi kuku kapona kideri
Ukisikia besidei basi tukutane sheli

Wananiita Sugu (nani)
Wananiita Sugu (nani)
Sugu Sugu Sugu (Rayvanny Boy)
Wananiita Sugu (nani)
Wananiita Sugu (nani)
Sugu Sugu Sugu

Niite Ray Sugu sungura mla dubu
Beat mama wa kambo ona linatema gubu
Mafuta na mashudu kipi unakihusudu
Vunja kibubu sije kuwa mchele ama gubu
Nafurahi kuona matusi ya wanaonipinga
Walio ninyima jero pindi na piga mizinga
Sasa na wapa kero zamu yao kuzinga
Talent kanipa Amila msistuke nikivimba
Uswazi ndipo napotoka sister du onyo kushoboka
Sitakuwa kuhonga iPhone nitakuhonga goroka
Simu ya kitochi ukacheze game la nyoka

Wananiita Sugu (nani)
Wananiita Sugu (nani)
Sugu Sugu Sugu (Rayvanny Boy)
Wananiita Sugu (nani)
Wananiita Sugu (nani)
Sugu Sugu Sugu

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU