MISTARI YA WIMBO HUU

Sifa ya moyo tamaa
Moyo sifa yake kutamani
Tamaa ya moyo
Inaweza kukuweka matatani
Unatamani kuzaa
Wakati bado uko shuleni
Tumia akili kukataza
Kabla hujawa matatizoni
Ile ndoto ya kitandani
Achana nayo
Kama unahisi labda haiwezekani
Kuendana nayo
Unaweza ukaota umejenga angani
Angani
Kuhifadhi ndoto ya shida gani
Wewe

Tuliza moyo wako
Kubali mapungufu yako
Rahisisha mahitaji yako
Ongeza kipato chako
Chunga tamaa mbaya
Chunga tamaa mbaya
Chunga tamaa mbaya
Chunga tamaa mbaya

Sifa ya macho kuona
Kutazama kinachoonekana
Ila sio kila unachokiona
Utadhani kupata inawezekana
Nyumbani kuna msichana
Njiani utaona wengi wasichana
Bora kuishia kutazama
Kuliko kujifanya unaweza sana
Siri ya maisha yako iko kwa muumba (muumba)
Alisema mbuzi ni mbuzi hawezi kuwa simba
Hawezi kuongea eti anaforce kuimba
Bora kutulia ama kupiga marimba
Utasikika pia

Tuliza moyo wako
Kubali mapungufu yako
Rahisisha mahitaji yako
Ongeza kipato chako
Chunga tamaa mbaya
Chunga tamaa mbaya
Chunga tamaa mbaya
Chunga tamaa mbaya

Mwanzo wa safari nakufuata kijana
Nakuja na swali unipe jibu la maana
Dunia bila wizi hivi itawezekana
Kama haiwezekani siku tukijaonana
Nitakiweka mbali kisimu changu cha Mchina
Vijana wote nitawaona hamna maana
Tunarudishana nyuma mambo ya kuibiana
Mwenzenu naona noma polisi kupelekana
Yeah

Tuliza moyo wako (tuliza moyo)
Kubali mapungufu yako (kubali kama vitu flani huwezi)
Rahisisha mahitaji yako
Ongeza kipato chako
Chunga tamaa mbaya
Chunga tamaa mbaya
Chunga tamaa mbaya
Chunga tamaa mbaya

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI