MISTARI YA WIMBO HUU

Nilishachovya matonge kwenye bakuli nyingi
Ila ladha nikakosa
Wapo walonipika na kuniunga, wapi sikuiva
Ila kwako nimechovya, nimetoweza kamwe sitotoa mkono
Kisomo nimesoma, we mwalimu nimefaulu yako masomo
Kikombe nipe maji ninywe nishibe namimi nikate kiu
Bila wewe chakula hakiendi nikila kitagoma kwenye koo
Heeh mamlaka ya wazazi wangu
Chanda chema kilale kwao
Ehe! wakisema nikipinga watahisi nawaona wajinga

Ooh!
Tuli tuli tulizana
Tuyaongee kwa kirefu na mapana
Ninayosema sijakudanganya
Na nikibisha sana nitapata laana
Tuli tuli tulizana
Tuyaongee kwa kirefu na mapana
Ninayosema sijakudanganya
Na nikibisha sana nitapata laana

Ohoo listen
Aaaamenituma mshenga, baba nae kanisihi saana
Baba nae kanisihi saana
Uuuh mtanashati kimwana aiseh kama mama kakupamba saana
Si unajua napendwa na wengi na wapo wanaoniwinda kwa pesa
Wakinipata dakika moja wananitumia kama dakika mia moja
Soo…

Tuli tuli tulizana
Tuyaongee kwa kirefu na mapana
Ninayosema sijakudanganya
Na nikibisha sana nitapata laana
Tuli tuli tulizana
Tuyaongee kwa kirefu na mapana
Ninayosema sijakudanganya
Na nikibisha sana nitapata laana

Naamini utakubali, kwa kheri na matumaini
Bila lolote shinikizo
Naahidi nitakujali, milele nitakuthamini
Hofu na huzuni kwako vitakwenda likizo
Anha wale wachache wenye vijimaneno watakuwepo
Wanadhani wanaharibu
Kumbe ndo kwanza wanafukuza upepo
Ohoo ehee
Wowowoh wowowooh

Tuli tuli tulizana
Tuyaongee kwa kirefu na mapana
Ninayosema sijakudanganya
Na nikibisha sana nitapata laana
Tuli tuli tulizana
Tuyaongee kwa kirefu na mapana
Ninayosema sijakudanganya
Na nikibisha sana nitapata laana
Tuli tuli tulizana
Tuyaongee kwa kirefu na mapana
Ninayosema sijakudanganya
Na nikibisha sana nitapata laana

Suddy Thomas!
Ngoma Records

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI