MISTARI YA WIMBO HUU

Ebwana siku hizi picha zangu siweki kwenye album
Sahivi ni mwendo wa selfie tu na ku-post Instagram
Ndo elimu yetu ya leo wanadamu
Ndo vile message ni WhatsApp,
Waga hatutumiagi kalamu
Mzungu katuweza
Sahivi ukisikia kizunguzungu ujue umeanza kuelewa Kingereza
Tanzania tunaweza
Japo siku hizi bila kuona uchafu kando ya lami huoni kama imependeza
Siku hizi usafi sio roho ni kutupia
Njia kuu sahivi mapenzi na sio njia kama njia
Ukiishi kwa kuhisi utajutia
Ila Peter anapopita ukibahatisha utamuita mpita njia
Najuaga Mungu ni wewe
Japo siku hizi watu wanaogopa ebola kuliko wewe
Kijana, mama ako hata kama mkiwa muelewe
Ndo mwanzo alirubuniwa kazini akupate wewe

Tusamehe Mola
Siku hizi watu wanaogopa Ebola kuliko wewe
Tusamehe Mola
(Najua si wakosefu wengi wetu twakukumbuka kwenye shida)
Tusamehe Mola
Siku hizi watu wanaogopa Ebola kuliko wewe
Tusamehe Mola
(Ujinga usio na hasara ni bora kuliko elimu isio na faida)

Huwa sipendi hangover
Nkishindwa kuikata na soda naikata na kiroba
Nasikia kuna Ebola mara kuna ngoma
Ila hakuna anaeogopa
Kuwa high sioni hatari
Kudadadeki
Nyonga kitu dry mpaka nikiongea sieleweki
Hakuna anaenidai
Sina kesi
Karibu uketi
Upate crate kisha ondoa hizo stress
Mishemishe zimekubali tuna-party siku kumi
Njoo uone watoto wakali wanavyocheza na wahuni
Na ukileta shari kuna ngumi hihihi
Jipange unaweza ondoka hauna kumi
Washa hookah washa fegi
Washa vuta washa change
Kinachofata hata sisemi
Alikuja na demu wake ataondoka ka kapuku
Eti kisa mbele ya watu aligoma kumpa busu
Mwaa mwaah

Tusamehe Mola
Siku hizi watu wanaogopa Ebola kuliko wewe
Tusamehe Mola
(Najua si wakosefu wengi wetu twakukumbuka kwenye shida)
Tusamehe Mola
Siku hizi watu wanaogopa Ebola kuliko wewe
Tusamehe Mola
(Ujinga usio na hasara ni bora kuliko elimu isio na faida)

Tusamehe Mola
Siku hizi watu wanaogopa Ebola kuliko wewe
Tusamehe Mola
(Najua si wakosefu wengi wetu twakukumbuka kwenye shida)
Tusamehe Mola
Siku hizi watu wanaogopa Ebola kuliko wewe
Tusamehe Mola
(Ujinga usio na hasara ni bora kuliko elimu isio na faida)

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI