MISTARI YA WIMBO HUU

Heyo Maneck..
Is mic on?
(Classic music)

Yoh!
Usingizi zaidi ya pono, dunia kwenye godoro
Ilompa bahari Dar kisha ikamnyima Moro
Ikashusha milima ambako Dar kuna kasoro
Kakupa wewe leo, mimi nangojea tomorrow
Kuwa tu binadamu tayari ni nusu ya uchizi
Sa unajua Mungu yupo, vipi unabeba mairizi
Vipi unakosa usingizi kwa maendeleo ya flani
Unampinga mpaka Mungu, hivi unajihisi wewe ni nani?
Wengi tulikuwa nao, leo hawapo mtaani
Uhai wa mgao kwenye kizazi cha shetani
Muumini ndo maibilisi, mwizi bosi wake polisi
Tanzania itachoka upendo utavunja ndoa na peace
Tatizo la wanasiasa love kwenye campaign
Wakishapata wanachotaka later people get pain
Kwa Mungu tuna madeni
Mama alisema nisifate dunia imebeba mengi

Dunia sio mbaya, walimwengu ndo wabaya ilo kila mtu anajua
Usimuone analia kivulini, ujue kabisa amechuma kwenye jua
Dunia imeharibika, dunia imechafuka
Siku nzima shika muziki
Tajiri na mali zake, masikini na watoto wake
Ona wanakufa na dhiki

Oh yoh
Cha ajabu pesa ina power na haizami gym
Ulimwengu umezidiwa madawa unapata wazimu
Nasali all night, nalala half an hour
Dhambi ni uchafu hautoki kwa kukesha shower
Hauogopi unapotea na bado Mungu anakulinda?
Huongopi kukosea na akili hazijapinda!
Unaeza ikwepa ndoa nyumbani kwako ila si msiba
Vipi Mungu akupe uhai, adhabu ukazilipie riba
Nani mwenye tiba ya ulimwengu wa majuto?
Dunia imemwagwa miba, binadamu kama puto
Kuiona siku mpya, naishukuru hiyo nafasi
Madaraja tu ya maisha, daladala wewe taxi
Mwenye nacho apewa tena na wengine hawana kabisa
Biashara zinafanyika misikitini na makanisa
Maisha magumu watu wamepoteza imani
Dunia imevua nguo mbele ya watoto wadogo mtaani!

Dunia sio mbaya, walimwengu ndo wabaya ilo kila mtu anajua
Usimuone analia kivulini, ujue kabisa amechuma kwenye jua
Dunia imeharibika, dunia imechafuka
Siku nzima shika muziki
Tajiri na mali zake, masikini na watoto wake
Ona wanakufa na dhiki

Yoh! Sometimes kulala naogopa (scared)
Nakuwa na hisia (scared)
Dunia imetekwa nyara na inabakwa kijinsia
Midundo masikioni ka malaika wananiimbia
Nashtuka niko ndotoni mapigo ya moyo yanakimbia
Sio wote walokufa hawajataka kupona
Sio wote waliopofuka hawajataka kuona (true that!)
Mlale salama mlokufa ajali ya Dodoma
Kilosa, Mbagala, Gongo La Mboto pia nimeona

Com, Roy, Vivi, Amina, Steve, John Mgema
Dj Kasanga, Father Nelly, Dandu mlale pema
We miss you, we love you all
(Dunia imeharibika, dunia imechafuka
Siku nzima shika muziki
Tajiri na mali zake, masikini na watoto wake
Ona wanakufa na dhiki)

Dunia sio mbaya, walimwengu ndo wabaya ilo kila mtu anajua
Usimuone analia kivulini, ujue kabisa amechuma kwenye jua
Dunia imeharibika, dunia imechafuka
Siku nzima shika muziki
Tajiri na mali zake, masikini na watoto wake
Ona wanakufa na dhiki
Dunia sio mbaya, walimwengu ndo wabaya ilo kila mtu anajua
Usimuone analia kivulini, ujue kabisa amechuma kwenye jua
Dunia imeharibika, dunia imechafuka
Siku nzima shika muziki
Tajiri na mali zake, masikini na watoto wake
Ona wanakufa na dhiki

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI