MISTARI YA WIMBO HUU

Eh
Watu wa ugali tembele
(Nahreel on a beat!)

Wanangu wote kule maghetto
Wanangu wote nyuma ya nondo
Wanangu wote kule maghetto
Wanangu wote nyuma ya nondo oh oh
Maisha ni hatua (pole pole)
Kwa mafanikio (pole pole)
Ukianguka inuka (pole pole)
Pole pole, pole pole

Umetoka nyuma ya nondo, holla!
Umetoka chini ya nini? Dola!
Segerea, Keko, wengine Mang’ola
Usogelee nini kingine? Mola!
Hakikisha unasitisha ukora
Kituo cha kati unarudisha bastola
Ufanye kiapo kwa sala hii
Jela ntolee, polisi ntolee
Uwizi ntolee, ubaya ntolee
Hapo kwenye menu niekee kazi
Niekee jasho, niekee uchungu
Niekee haki, niekee Mungu
Aliye juu, aliye niamini
Usirudi jela hallelujah, amini

Wanangu wote kule maghetto
Wanangu wote nyuma ya nondo
Wanangu wote kule maghetto
Wanangu wote nyuma ya nondo oh oh
Maisha ni hatua (pole pole)
Kwa mafanikio (pole pole)
Ukianguka inuka (pole pole)
Pole pole, pole pole

Eh
Watu wa ugali tembele (pole pole, pole pole)

Chalii jela hauwezi lala chali (chalii)
Jela huwezi pata zali (chalii)
Kuta huwezi kuona mbali, chalii
Hujawahi lala hata mlango wazi chalii
Leo unalala na majambazi chalii
Na diko ni moja kama futali chalii
Narudi kijijini kumuona babu na bibi
Narudi kanisani kusali sala ya ushindi
Narudi msikitini kupigania misingi
Narudi darasani kusoma hesabu kwa bidii
Usirudi jela, usirudi tena
Usirudi chini, usirudi tena
Tufanye kiapo kwa sala hii
Jela ntolee, polisi ntolee
Ubaya ntolee, wizi ntolee
Hapo kwenye menu niwekee kazi
Niwekee jasho, niwekee uchungu
Niwekee haki, niekee Mungu
Aliye juu, aliye niamini
Sirudi jela hallelujah, niamini

Wanangu wote kule maghetto
Wanangu wote nyuma ya nondo
Wanangu wote kule maghetto
Wanangu wote nyuma ya nondo oh oh
Maisha ni hatua (pole pole)
Kwa mafanikio (pole pole)
Ukianguka inuka (pole pole)
Pole pole, pole pole

Eh
Watu wa ugali tembele
Eh eh
Watu wa ugali tembele

Wanangu wote kule maghetto
Wanangu wote nyuma ya nondo
Wanangu wote kule maghetto
Wanangu wote nyuma ya nondo oh oh
Maisha ni hatua (pole pole)
Kwa mafanikio (pole pole)
Ukianguka inuka (pole pole)
Pole pole, pole pole

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI