MISTARI YA WIMBO HUU

Nana na nana
Nana nana na na
Nana nana na na
Wee mama wee (chapa)
Nana nana na na (chapa)
Nana nana na na
Nana nana na na (Tongwe Records baby)
Wee mama wee
Nanana wee nana wee
Nanana wee nana wee
Nanana wee nana nana
Wee mama wee

Nimeshapigwa sana mkwara na jumbe za vitisho
Ila siamini huu msafara ni vibaraka wa Mrisho
Si tulianza sawa vita ya kuitetea ikulu
Leo umeisaliti UKAWA kwenye sherehe za uhuru
Uhuru uko wapi
Mnasherehekea uhuru
Uhuru wa kutowafilisi viongozi wakijiuzulu
Na wanaokufa maskini wanangu wa Burya Nkulu
Mungu aliwapa madini mnambinafsisha Mkaburu
Bungeni sioni kinachoendelea
Naona wasomi wakisutana umbea
Wengine walishikwa ugoni picha zilienea
Hamuwaoni jimboni afu bado mnawalea
Mambo yaki** spika anabadilisha mada
Akiona chama tawala amedhalilishwa kada
Spika wa bunge ona analinda watu wa chama chake
Na bunge ni la watu wote sio chombo cha watu wachache
Safari ya raisi eti tume inaundiwa tume
Wakati Mwananyamala wanatibu tezi dume
Kadi chama nachana nanyongea ganja navuta
Nikamateni si mlimshindwa Tibaijuka
Leta Defender leta wajeda leta wagambo Roma nimejitoa sadaka
Na mkitaka kuniua hiki kichwa sifii hapa
Nichinjeni mkanitupe kwenye daraja la Mkapa
Motherf*cker walafi wa madaraka
Hata Nyerere Gaddafi si walikufa kwa mashaka
So hakuna kiongozi msafi
Je nani mwenye mamlaka
Anitajie mtoto wa raisi anayesoma shule ya kata

Viva Roma viva viva Roma viva
Viva Roma viva viva Roma viva
Bendera bendera
Bendera bendera
Bendera bendera
Wee mama wee

Katiba ni sauti ya umma na kuna uhuru wa kuongea
Na nyie si ndio mmenituma mpo tayari kunitetea
Wilaya mnafanya mkoa ili wapangwe washkaji
Mkuu wa wilaya changudoa hii ni miradi ya upigaji
Watasafirisha nyani sisi tunashangaa twiga
Utamfunga nani Yeye na mwanasheria mkuu ni maswahiba
Na wasanii tuombee raisi ajaye asipende tu vikuu
Wataalikwa wapemba hatutamuona hata Lukuvi
Unampigiaje kura fisi awaongoze mbuzi
kwa hongo ndogo ya kipisi unampa ikulu mlanguzi
Geita mlinyimwa dhahabu watawalaghai kwa vitenge
Napata ghadhabu propaganda za wabunge wase ngerema
Ukistaajabu ya Lema utayaona ya Mrema
Ona pepo la usaliti linaitafuna Chadema
Kwetu raisi ni taasisi inayochaguliwa na mfumo
Sisi wawakilishi na kwenye maamuzi hatumo
Watoto wao wanauza ngada baba Fisadi
Mama anafanya ukahaba yupi mwema kiitikadi
Na vita ya mahakama ya kadhi ni uhasama wa wazi
Yaani unaisaka bikira ndani ya wodi ya wazazi
Nipige risasi ya utosi si ndio nidhamu ya utawala
Maana waliomuua Mwangosi waliongezewa mshahara
Dokta Mvungi ona dah
Wakamzawadia jeneza na hawafungwi
Nipe kesi nitaimba ndani ya gereza
(Peperusha bendera)
Mbona mama yako anauza gongo na gongo ndio imekulea
Hadi leo umekuwa polisi na humpeleki Segerea life is not fair
Polisi mna maisha gani
Mnakufa masikini kwa kuwatetea wanyang’anyi

Peperusha bendera
Viva ROMA Viva
Peperusha bendera
Viva ROMA Viva
Peperusha bendera
Viva ROMA Viva
Peperushaa aya iyaa
Bendera bendera
Bendera bendera
Bendera nana nana
Wee baba wee

Hakuna mtoto asiye na mzazi yupi wa serikali ya tatu
Mikataba iweke wazi demokrasia ni watu
Ona sasa kila msomi anaikimbilia siasa
Nchi itajengwa na nani Ajira imekuwa serious
Wanafanya biashara haramu bado hawalipi kodi
Nani atahoji Na wao ndio wadhamini wa bodi
Jasho analila mzungu wachimbaji wadogo wa migodi
Au mnataka Ivan aje awe mfuasi wa panya road
Pesa starehe za muungano hamzingatii itifaki
Wanafunzi mnawachoma jua na shule hawana madawati
Mnalipa mishahara hewa na hamlipi mafao walimu
Na mlimpiga Warioba alivyowaletea rasimu
Nchi inalima pamba nyinyi mmeua viwanda
Tunauzia wawekezaji ona doller inapanda
Tunageuka waagizaji kisha wanatuuzia mitumba
Uchumi unayumba leta fujo upigwe kama Lipumba
Nakutabiri nani afuate Karibu Tanga kunani
Huku hatuitaji kakakuona wala pweza wa ujerumani
Round hii kombe linaenda Monduli (Masai yelo subhai)
Au kombe ni la Magufuli
Kama kawa kama dawa je kombe linabaki Ukawa
Mmarekani anataka wese (we hakuna atakayepona)
Na mchina akifuata gesi Mwambie nangwanda sijaona

Viva Roma viva
Viva Roma viva
Viva Roma viva
Wee mama wee

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI