MISTARI YA WIMBO HUU

Mwenzenu kichwa maji mpaka walimu wamenichoka
Nitarudia la nne mpaka midevu itanitoka
Sijui ubishi unachangia? Siku ya usafi sina maji wala mbolea
Minywele tim tim, shati sijachomekea
Mguu wangu unanibeba, walimu hawataki kunipiga
Kesi mwanafunzi Chiba
Masomo siyatamani, mapumziko niko nyumbani
Mama kantuma mchele, nimerudi na unga
Ona, kanipa kikaratasi ili nsisahau tena
Naenda huku naimba ‘mchele robo, mchele robo’
Pita huku, tokea huku ‘mchele robo, mchele robo’
Mama! Nimenunua nusu

Kichwa changu mbumbumbu
Naambiwa sasa hivi, baadae sina kumbukumbu
Shuleni zero, nyumbani zero
Mitihani zero, kichwa changu zero, zero!

Tumeruhusiwa mapema mama, shuleni kuna maafa
Mwanafunzi kagongwa na gari, mwalimu mkuu kafa
Inatakiwa michango kila mwanafunzi efu sita
Tupeleke wanafunzi, wazazi nyumbani kupumzika
Sijali, sipeleki shuleni, msiba kwenye kamari
Asofunzwa na mamaye, hufunzwa na ulimwengu
Sikumsikia mama nilitukana walimu wangu
Leo najuta, naokota machupa
Nilosoma nao mambo super
Kibao kimeandikwa hamna njia, mi napita

Kichwa changu mbumbumbu
Naambiwa sasa hivi, baadae sina kumbukumbu
Shuleni zero, nyumbani zero
Mitihani zero, kichwa changu zero, zero!

Wanafunzi halelu.. eti haleluya!
Wanafunzi habari zenu? (Nzuri, shikamoo mwalimu)
Haya, Kidako jana tulijifunza somo gani?
Mdahalo
Wanafunzi pigeni vigeregere.. ma.. makofi kwa Kidako
Haya, we Chiba Wa Ajabu.. (jana na leo)
Hebu tueleze jinsi gani ya kuandaa mdahalo
Asante mwalimu, jinsi wa kuandaa mdahalo wako (enhee)
Unachukua sufuria, unaweka jikoni
Unachukua mafuta, unaweka kwenye sufuria
Yakichemka, unachukua mdahalo wako unaweka kwenye sufuria
Baada ya dakika thelathini, unakuwa umeiva mdahalo wako
Unauipua, uko tayari kwa kuliwa
Asante mwalimu
Haloo nikamatie huyo mtoto
We hebu kaa.. kaa.. huyo alaa.. anapuluchuka huyo, wee! Mkamate!

Kichwa changu mbumbumbu
Naambiwa sasa hivi, baadae sina kumbukumbu
Shuleni zero, nyumbani zero
Mitihani zero, kichwa changu zero, zero!

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI