MISTARI YA WIMBO HUU

Baby mooh nifanye Big G unitafune
Ama niwe sindano nawe uwe uzi nguo nifume
Ama niwe ndoo uwe maji yangu unawanume
Nifanye kucha kama ukiwashwa mi nikukune sema mama

Niwe duka la vipodozi nikuvutie kwa kila kitu
Chumbani uwe simu unalia hata nikikubipu
Nisimame kama kinyozi nikikunyoa unanisifu
Niwe godoro na shuka nilale na wewe kila usiku

Shika ufunguo gari ya bosi wangu
Kwako zezeta zezeta
Niko radhi nifunge ule wewe
Mimi zezeta zezeta
Au unataka hati nyumba ya baba yangu
Kwako zezeta zezeta
Kifaranga nibebe kama mwehu
Mimi zezeta zezeta

Mama sitaki paka na panya vita za nini
Mi nataka niwe mafuta ujipakaze kote mwilini eeh
Ama niwe taulo kanga laini ukioga ninakufuta
Kutoka juu mpaka kwa chini mashallah
Ulivyo mwenzako taabani naishi muchumba siendi varandani
Tena sikufanyi vocha soko dukani
Nikutumie muchumba nikutupe jalalani sema mama

Niwe duka la vipodozi nikuvutie kwa kila kitu
Chumbani uwe simu unalia hata nikikubipu
Nisimame kama kinyozi nikikunyoa unanisifu
Niwe godoro na shuka nilale na wewe kila usiku

Shika ufunguo gari ya bosi wangu
Kwako zezeta zezeta
Niko radhi nifunge ule wewe
Mimi zezeta zezeta
Au unataka hati nyumba ya baba yangu
Kwako zezeta zezeta
Kifaranga nibebe kama mwehu
Mimi zezeta zezeta

Mashilawadu
Wananyapia nyapia
Mashilawadu
Wananyatia nyatia
Mashilawadu
Wapate kutangazia
Mashilawadu
Kuwa makini mama
Mashilawadu
Kwa kudandia dandia
Mashilawadu
Vya watu kupagazia
Mashilawadu
Macho funika pazia
Mashilawadu
Kuwa makini mama eeh eeh

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI