MISTARI YA WIMBO HUU

Zimbabwe – ROMA

Wengi mlijiuliza walioniteka ni maaskari
Mkanitafuta vituo vyote Cetral hadi Sitakishari
Wakasema hawajui nilipo mama alienda mpaka monchwari
Daaah
Ya Kaisari mwachie Kaisari
Machozi yenu yatalipwa mimi nafunga na kusali

Imba Roma imba
Imba Roma imba
Imba Roma imba

Mungu wa Paulo ndio mungu wa Daudi
Na ndio mungu wa John mnaemuita Yohana wa Wayahudi
Mwanangu alimuuliza mama “Baba lini atarudi”
Na mke wangu aliwaliza kuwashukuru sina budi
Fahamu ya kuwa mimi sio tu rapper
Mimi ni baba wa familia
Na watoto mahitaji nawapa kama isemavyo Biblia
Kipi bora
Nife mseme nilikufa kiharakati
Siogopi kufa ila nawaachaje wanaobaki
Je nani kati yenu mwanangu atampa malezi
Wapi atapata mahitaji
Wapi atapata mapenzi
Mama nae wapi atapata mahitaji na malezi
Na report ya upelelezi vipi aliiteka mtekaji
Je kaburi langu mtalipalilia majani
Nimeumwa hamjakuja kuniona mnangoja mje msibani
Nilipokuwepo sikuwa najua hii saa nne
Hii Saanane
Nilichohitaji nitoke mzima na ndugu zangu tuonane
Nimechapwa mijeledi nimevunjwa bila huruma
Asante mliopaza sauti nimeiona nguvu ya umma
Siku tatu nimefungwa macho mikono imefungwa nyuma

Nakwenda Zimbabwe
(Zimbombo iyelele mama we)
Nakwendaaa Zimbabwe
(Zimbombo iyelele mama we)
Nakwenda Zimbabwe
(Zimbombo iyelele mama we)
Nakwenda Zimbabwe
(Zimbombo iyelele mama we)

Imba Roma imba
Oo
Ee mama (sema baba wewe)

Nasimama na naunga hoja kwenye uchumi wa viwanda
Nanasi linauza Msoga tikiti linaoza shamba
Walioniteka hawakuja na Noah
Ni uvumi na visanga
Ila kutekanateka huu ni uhuni wa kishamba
Weka bunduki chini si tubishane kwa hoja
Maana sote lengo letu kuijenga Tanzania moja
Mi sikuona nyota kwa shoulder
Ila najua wewe ni soldier
(Inshallah)
Ulikuja mwenyewe ama ulipewa order
(Hewallah)
Aminini siku hazigandi wewe ni Yanga mimi Simba
Kwa mpinzani sio dhambi
Ipo siku mtawala atakuwa mpinzani
Simba akichukua kombe sijui atapona nani
Na kuna mbunge alisema eti nimemtukana mkuu
Utahukumiwa na mkono wa Mungu
kumshtakia aliye juu
Kwanza lini
Na kwanini mimi nimtukane mjomba
Umepewa gari ya wagonjwa mi Tanga wananijalia bomba
Mimi mbarikiwa na nikifa nitaketi kuume kwa baba
Na ni mtu wa watu that is why lilisimama bunge la bajeti kunijadili
Mtanzania kuwa makini pia makinikia nayatungia
Mapini Piya
Nilitabiri utaitwa Raisi kipindi unaitwa waziri
Japo maisha sio rahisi japo pongezi unastahili
Waliosadiki Roma ataonekana kabla ya Jumapili
God bless imetimia injili nilio itabiri

Nakwenda Zimbabwe
(Zimbombo iyelele mama we)
Nakwendaaa Zimbabwe
(Zimbombo iyelele mama we)
Nakwenda Zimbabwe
(Zimbombo iyelele mama we)
Nakwenda Zimbabwe
(Zimbombo iyelele mama we)

Imba Roma (ee ee Roma)
Zimbombo we simama (ee ee Roma)
Sema baba wewe (ee ee Roma)
Iyelele mama wewe (Zimbombo we simama)
Watakwenda huko Zimbabwe
Ee ee Roma (iyelele mama wewee)

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU