MISTARI YA WIMBO HUU

Hahahhaa
13
Bongo Records

Mama ndiye alinitabiri mi nitakuwa staa na nyota kila pande
Nikiwa na raha kama nina hasira nisijigambe
Usimpige mkeo piga shangwe
Maana Young Killa sio ngazi kwa hiyo mwambieni shetani asinipande
I think big is my dream big kuwa bigga wa michano
Ni**a ambae tajiri atanijua kuwa msodoki nawaficha mistari
Upeo wangu umekula mchicha na ndiyo maana nna fikra za kuona mbali
Msukuma naye sukuma mitikasi inatulia
Hata Francis Cheka naweza mpiga punch akalia
Wanayoijua njaa ndiyo wanaamini cha kwanza kilimo
Mi sitaki gombania u-star ili nikifa nikazikwe kino
Wabovu wakichana imoo na hawajui nguzo tano
Leo kwenye u-star simo kisa sina muonekano
Mi nna-power ya ibada niliyo iomba baada ya kuipata
Pole dada ulienitosa kisa umenizidi kidato
Futa jasho na damu saka noti hali tete
Watoto wanamjua Diamond na joti zaidi ya Kikwete
Popote niko fiti tega sikio
Shoga hata akitoa jicho vipi hawezi akayaona mafanikio ndiyoo

Msodoki na Ngoshaa
Ndiyo miujiza iliyotabiriwa
Haina haja ya kuogopa
Nafasi nilizozichezea yawezekana zisirudi
Lakini naweza zitengeneza nikiongeza juhudi
Tangu Agosti Tangu Aprili 13
Tangu Agosti Tangu Aprili 13
Na-hustle bila wasi wala hofu
Ubongo hauwezi nipa shida ambayo ntashindwa kuisolve

Wakishaamini unawahitaji zaidi ya wanavyo kuhitaji
Mapenzi ya wadau wa mjini hugeuka samaki na maji
Kuishi ndani yake tu nje yake uvuliwe
Kwa msaada wake upigwe kisha anawishe uliwe
Sikuumbwa nije ku-settle for less
Naisubiri mvua inyeshe nijitokeze ku-dance
Non sense sitemi asset siyo deni
Homeboy natema vitu on point jifunzeni
Thamini huu muda kabla hujageuka history
Part of the past don’t fit the script for the future memory
Niliyo ya pitia yameniandaa kwa haya yajao
Siyo dalili ya kusinzia ni njaa nikipiga mihayo
Sina jeuri wala mzaha kugeza tabia mbovu
Nna kiburi cha jeraha ukinipoteza naacha kovu
Maskini najiamini hadi natokwa na ukungu
Bila ujuzi wasinge ni thamini ningetoswa mpaka na ndugu
Kitacho nizamisha siyo kudondoka mtoni
Ni kushindwa kupiga mbizi nakusizi ili msinione

Msodoki na Ngoshaa
Ndiyo miujiza iliyotabiriwa
Haina haja ya kuogopa
Nafasi nilizozichezea yawezekana zisirudi
Lakini naweza zitengeneza nikiongeza juhudi
Tangu Agosti Tangu Aprili 13
Tangu Agosti Tangu Aprili 13
Na-hustle bila wasi wala hofu
Ubongo hauwezi nipa shida ambayo ntashindwa kuisolve

Napenda umaarufu nachukia mbwembwe zake
Unapospit truth kwa boothe afu wa-kush hamninyaki
Nawaacha uchi ukweli uzushi siyo mwake
Hata mkighushi mtafeli hamnigusi na hamnipati

Siamini nimekuwa mimi hadi leo nimefika hapa
Alionilea hakuniamini niliyemtegemea hakunitaka
Bila nyinyi wadau nakiri sishiki sarafu
Na ndiyo maana sili bata kwa maana bata wachafu
Kuwa mkali wa kusifiwa kubali kutumiwa
Nilichoambiwa kuwa siku hizi hadi wajanja wanaliwa
Inatakiwa kuwa streka mambo yaende shkopa
Kama hujanileta huwezi nirudisha nilipotoka

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI