MISTARI YA WIMBO HUU

Tanzania eeh
(Tongwe Records Baby)
Nchi yangu ohh

Huwezi kuijenga Roma haikujengwa kwa siku moja
Iwe kwa raha leo au simba mtoto tanga watakuja
Hata pacho pia ni mwamba ila bado anakata viuno
Kaskazini bila tanga ni msondo bila Gurumo
Alisema juu ya mwamba atalijenga kanisa
Na halitatikisika waumini tuianze misa
Kwenye njaa kula kuku aliyechinjwa na padri hewallah
Adhana ikilia amka ukamuombe Allah
Bwa Shehe mrudie Mungu Masanja kawa mchungaji
Sujudu Mecca madina tajiri hataki kuhiji
Maulid Ubungo Kibangu ndo mishahara ya madrasa
Ona rafiki wa padri kawa muhasibu wa kanisa
Tenda wanapeana kindugu mwanangu kua uyaone
Familia ilikata ringi na mama alibaki mjane
Sikuwa na damu ya kiarabu kwamba nitayarithi mabasi
Dingi hakutupa msingi ona gari twaifanya taxi
Tazama Gongo La Mboto mtoto kamzaa mtoto
Na atalelewa na nani baba ‘ake mmemfunga Keko
Wape buku waue winga wale watoto wa Morocco
Mungu atazidi kukulinda kesho utaiona sabato
Mzee wa bandari kastaafu kajenga banda la uani
Ana wake wa tatu je watoto watarithi nini
Ndo chanzo cha kurogana na kutupiana majini
Huyu akimpandisha Makata yule Maimuna Subian
Maana pesa ndo ilifanya tusiwe na Tanga ndugu
Pesa ilileta ubaguzi kati ya Loyola na Pugu
Pesa ndo ilichochea beef ya Nice na Dudu
Na pesa ndo ilimaliza vita ya Ruge na Sugu

(Tanzania eeh)
Mwanangu kua uyaone
Kama ntawahi kuiona paradiso mtunze mama ‘ako
(Nchi yangu ohh)
Mwanangu kua uyaone
Marahemu hufa na chake pigana upate chako
(Tanzania eeh)
Mwanangu kua uyaone
Mwalimu cheza kibati wanao wasife njaa
(Nchi yangu ohh)
Mwanangu kua uyaone
Elimu imekosa thamani Necta ivuja kibaha

Aminini nawaambieni ujana ni maji ya moto
Mtoto humzika mama leo mama anamzika mtoto
Ndo maana mama alisema nisimchumbie mmachame
Muraa shusha mapanga naileta posa Tarime
Leo bahari imechafuka mpemba haishemu karafuu
Hatari kama Nungwi nahodha sio Kirikuu
Yakhee nirushie mtumbwi mie mwamba sio kichuguu
Hii ni vita ya msambaa mbondei usitie maguu
Ona kipindi cha bunge Dodoma inanuka ngono
Spika akiahirisha bunge wengi watau-support mgomo
Wabunge mnadai posho muhonge dada zetu
Kuna wanafunzi wa mama Salma vyuoni usicheze peku
Wazanzibari hawaioni thamani ya huu muungano
ila kulichoma kanisa sio njia ya kuvunja agano
Sioni sababu ya ubaguzi na kuua wasio na hatia
Wakati aliochanganya mchanga mchanga umeshamfukia
Muislamu gani unahonga bongo movie mamilioni
Mama anakufa Mwaisela kakosa dripu ya quinine
Ni heri ujenge msikiti tuitukuze mitume
Anasa za bakulutu unatunza wacheza sebene
Unamuheshimu Ramadhani unazini mbele ya Shaban
Kama ilishushwa Quran twendeni misikitini
Anaedhihaki msahafu pengine kanisa halijui
So kulichoma kanisa ni kuuza Bible Dubai
Usihofu kumpoteza mmoja ili kumi waishi vema
Watanzania tuna uoga sio amani mnadanganywa
Sacrifice for your son and daughter amka kifikra
Damu yako iwe chachu ya ukombozi dokta Ulimboka
Mkinga usimuue mama ili uongeze kipato
Utajiri upo kaburini watu wamekufa na ndoto
Leo Ridhiwani haufanani na Makongoro dah
Sina hela ya kiroba Rashidi nigongee ugoro
Suka kaiangusha lori ya mafuta yote magendo
Waziri anaziuza pembe za ndovu na meno ya tembo
Nchi imejaa misitu tuna uhaba wa madawati
Tunakula vitu feki TBS mko wapi
RPC usitume kikosi ili uishushe Chadema
Italipwa damu ya Mwangosi Iringa semeni amina
Okoa wagonjwa wa saratani mpakani zuia wakimbizi
Kuliko kumwaga pesa kwenye tume za uchunguzi
Muhimbili naumwa goti eti dokta kapasua kichwa
Mbeya wanapigwa nyundo ili raia wauze mabucha
Amana wanatelekeza watoto wanalia Mwananyamala
Wanatuua na hawaendi jela jela anakwenda Kajala

(Tanzania eeh)
Mwanangu kua uyaonee
Meshii acha kisirani gonga muhuri tuwahi
(Nchi yangu ohh)
Mwanangu kua uyaone
Traffic hasira za mkeo barabarani hazifai
(Tanzania eeh)
Mwanangu kua uyaone
Wanahonga mashabiki ngoma zao wazi-request
(Nchi yangu ohh)
Mwanangu kua uyaone
Udini wa ma-presenter wapagani unatu-cost

Sauti hii itasikika mpaka Oldonyo Lengai
Nikifa naomba nizikwe Tanga na mje kwa Shambalai
You can kill me bro but You won’t kill what I’m standing for
Usiutamani urithi wa baba ikimshuka CD4
Eti tuzo sikustahili haa haaa hii ni hatari
Tuzo ina chapa ya nani Ya Kaisari mpe Kaisari
Hii sio Masaki ni Ngaramtoni mama anaiuza dadii
Muziki umejaa stress kila nyumba ina msanii (woyoo)
Yanga wamemfukia mbuzi golini simba ana bundi
Viongozi wanataka umate umate hawaujali ushindi
Utawasikia Chuji kachuja kiburi choma mahindi
Kapigwa ligi ya jogoo shahidi kamati ya ufundi
Vijijini tupo wengi mleteni daktari bingwa
Ana ngoma utasikia kalogwa twende kwa mganga
Pesa za kujikimu ndo ulichongesha kitanda
Kulea mimba sio mchezo ba kijacho haujajipanga
Professor kanyimwa penzi utasikia Carol kadisco
Carol analea ndugu kwa pesa ya bodi ya mikopo
Poleni mnaotafuta C mwaka wa 4 mna risiti
Huku headmaster kaenda mjini eti shule imeishiwa chaki
Msiwaue wachimbaji wadogo Geita inalia
Kaburu umempa migodi UDSM tuna engineers
Unapewa kontena la condoms uionge dhahabu
MV Spice ilipozama TV inaonyesha Taarabu
Kamanga hawaiweki lami ili tuvukie Busisi
Dereva usinitoe kafara ili utimize hesabu ya boss
Sina cha kuweka rehani kwenye asasi za mikopo
Bajeti ya kilimo kwanza mkulima silioni soko
Tanga mmekosa nini amkeni acheni umwinyi
Hawa wachaga hawatuwezi ona Manka bara 20
Bandari Chanu Relwe chali Makamba iinue katani
Zito akiroga Kasulu si tunamrogea Pangani
Uchafu wa Mrisho unafanya msafi aonekane Benja
Msisadiki magazeti waandishi wengi kanjanja
Vijana ndo nguvu kazi ila wengi wamejaa Lutindi
Mitaani wamekata ringi hadi figo wanaziweka bond
Majibu ya postmotam ameshayanunua wakili
Na hakimu kapewa kiwanja Kimara apige kufuli
Cheki dola wanainunua kesi napewa kapuku
Nawa mpole kama ngamia mbele ya hakimu wa Kisutu

(Tanzania eeh)
Mwanangu kua uyaone
(Nchi yangu ohh)
Tongwe Records

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU