MISTARI YA WIMBO HUU

Adhabu ulonipa sio sawa yangu
Mpenzi umeniacha bado nakuhitaji
Bwana ulompata anakudanganya
Adhabu ulonipa sio sawa yangu
Mpenzi umeniacha bado nakuhitaji
Bwana ulompata anakudanganya

Asubuhi imefika na jogoo ndo anawika
Naamka mchovu kitandani mpenzi wangu sikuoni
Nafanya usafi chumbani kwetu
Naikuta barua ah chini ya mto wako
Juu umeweka wig lako
Ili isipeperuke
Taratibu naifungua
Umeanza na kusema
“Darling darling hallo
Hallo mpenzi hallo”
Na makiss ya kumwaga
“Nia na madhumuni ya barua hii
Ni kukujulisha kwamba
Mimi na wewe basi basi basi
Naomba usinielewe vibaya
Naomba usinichukie mpenzi
Nakuomba mpenzi uisome kwa makini tafadhali eh”

Adhabu ulonipa sio sawa yangu
Mpenzi umeniacha bado nakuhitaji
Bwana ulompata anakudanganya
Adhabu ulonipa sio sawa yangu
Mpenzi umeniacha bado nakuhitaji
Bwana ulompata anakudanganya (anakudanganya)

“Nimempata bwana wa kizanzibari
Anaejua mapenzi mwenye sifa zote
Mwenye pesa zake na usiku naolewa ah”
Nilikunyima nini mpenzi wangu Mariam
Kama ni mapenzi Mariam nilikupa
Nyimbo zote nikakuimbia
Kizazi ninacho
Unachotaka ni nini zaidi ya utu wangu mpenzi wangu
Kumbuka ya kwamba kwa mara ya kwanza maishani
Ni mimi niliyekutolea damu
Ulipokuwa mahututi kitandani
Ndugu zako wote walikuwa bize
Nikajitolea kwa mara ya kwanza mpenzi wangu
Mariam chozi langu la mnyonge
Malipo ni kwa Mungu mpenzi Mariam
Mariam oh Mariam wewe
Unaenifanya nikuimbe kila siku Mariam eh

Adhabu ulonipa sio sawa yangu
Mpenzi umeniacha bado nakuhitaji
Bwana ulompata anakudanganya (anakudanganya)
Adhabu ulonipa sio sawa yangu
Mpenzi umeniacha bado nakuhitaji
Bwana ulompata anakudanganya (anakudanganya)
Adhabu ulonipa sio sawa yangu
Mpenzi umeniacha bado nakuhitaji
Bwana ulompata anakudanganya (anakudanganya)
Adhabu ulonipa sio sawa yangu
Mpenzi umeniacha bado nakuhitaji
Bwana ulompata anakudanganya (anakudanganya)

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI