MISTARI YA WIMBO HUU

Farid Kubanda alizaliwa August 13
Katika hospitali ya Bugando iliyopo jijini Mwanza
Sababu mtoto kwa mama hakui alilazimika kulelewa na bibi yake
Na ilikuwa ngumu sana kwa bi mkongwe huyu kugundua ndoto za huyu mjukuu
Mara kwa mara alimkuta kufungulia mziki
Halafu kama anaongea peke yake hivi
Bibi alihisi labda jamaa ana matatizo ya kiakili
Na kuamua kumripoti kwa mama yake mapema
Kabla haijawa aibu mbele ya elimu za kila tawi
Hawakujua
Hawakujua
Huyu hapa

Na hisia ka za Bob Marley ila sifanani hata na Zigi
Tangu Agosti 13 niliyozaliwa nikajiita Fid
Kwenye ukoo wenye chapaa kama yuko bosi wa Zumo
Ukatokea wakati wa njaa ulipotokomea wa mavuno
Dingi haonekani nyumbani majukumu yote mama ‘angu
Nimeona nimejifunza mengi kwa kujiongeza kivyangu
Sasa usiukaze msuli kama upaja wako mdogo
Na usitanue miguu Fid Q atakupiga tobo
Nashangaa mnaleta shobo ukweli mnageuza uongo
Nyie petroli mi ni moto
Kunizima bado ni ndoto
Mwanaharakati kama Mkapa shingoni nina chain ya gold
Moyoni mi ni hardcore usoni nioneni bishoo
Hamjui nilipotoka labda hapa nilipo
Na Mungu ndiye pekee ajuae lini ntafika mwisho
Sijafikia hatua ya kuitwa bosi nami nikaitikia ndio
Lakini naweza kumpa maji mshikaji yeyote aliye na kiu
Sijaribu kupima kwa shingo ukali wa upanga
Au kuimba huku natafuna karanga
Au sumu kwa kuilamba
Maneno mkuki hekima ngao
Na hizi chuki kama hawaelewi
Na isitoshe wajuavyo wao ni tofauti sio kivile
Fid ni jeshi la mtu mmoja ambaye hajafeli mtihani wa mziki
Street naitwa Ngosha The Don hamnitishi nyie ma-snitch
Sasa ombeni mvua msiombe ujio wa mie Katrina
Ni zaidi ya mafua ya ndege hofu ya dunia nzima
Usijifanye una ngozi ya chuma ukiguswa inabonyea
Kurudi nyuma naona mbali bora mbele kuelekea
Fid Q mwanahisabati mi ndo mkuu asiyeshikwa shati
Muigiza jiti ka Daudi tayari kwa kumuua Goriati
Nshafukuzwa na ndugu kosa nilisahau kusuuza sahani
Nikaenda kuishi kwa mshikaji flani huko nako sikuwa na amani
Kwa kuwa niliamua kuamini pasina kuwajua kiundani
Kwa makosa ntajifunza na sintowasahau

Nipo duniani tangu Agosti 13
(Kiubishi ubishi)
Navuja jasho kimpango wangu
(Nimejifunza)
Maisha ni shida na raha
Kuna starehe na karaha
Utachekwa ukizubaa

Nipo duniani tangu Agosti 13
(Kiubishi ubishi)
Navuja jasho kimpango wangu
(Nimejifunza)
Maisha ni shida na raha
Kuna starehe na karaha
Utachekwa ukizubaa

Matumizi bila akiba pesa zitatukimbia
U-superstar ni mzigo wa mwiba ukiubeba unaumia
Hii dunia ina mambo kama wasemavyo Watu Pori
Ndo maana nikiwa na mpira basi kinachofata goli
Ujanja ukiuzidisha si muda mfupi utaitwa mshamba
Alianza rap enzi hizo Sinza watu wanauziwa viwanja
Unga ukamfunga kamba isiyokatika pembamba
Mwenzetu yu ndani ya giza anauliza uwapi mwanga
Sasa kwa ubishi na hasira kama Squiza mimi naja
Kwa ushindi wa haja kama uvunjiko wa bawaba
Nikienda chimbo haipiti wiki yaani haizidi siku saba
Huyu jamaa anaitwa muda sio rafiki wa mwanadamu
Atakukosesha mavumba kama hauko on time
Amenyae kwa mdomo siku zote haishi kutema
Asante Mungu kwa hii sauti yenye busara leo nasema
Maisha ni kama kioo ukiyachekea nayo yanacheka
Na hii mipaka bila uhuru Afrika ni utumwa wa kifikra
Chagua ufe kiujerumani uanguke na tai shingoni
Au mchaga anayeshinda njaa wakati anazo hela mfukoni
Huu sio muda wa kujaribu wenzako wanafanya kweli
Au hujui bahari tulivu haimbiri nahodha wa meli
Ona wasio na hatia wanapelekwa gerezani
Halafu wavunjaji wa sheria wanaachwa wajazane uraiani
We unadhani nuru bandia za shetani zitaharibu imani
Za wale wanaougua na kulia juu ya makosa ya mtu fulani
Maneno yangu mi ni ya moto
Na mdomo wangu hauna friji
Yanantoka bila kuyapoza nauliza niliyameza vipi

Nipo duniani tangu Agosti 13
(Kiubishi ubishi)
Navuja jasho kimpango wangu
(Nimejifunza)
Maisha ni shida na raha
Kuna starehe na karaha
Utachekwa ukizubaa

Nipo duniani tangu Agosti 13
(Kiubishi ubishi)
Navuja jasho kimpango wangu
(Nimejifunza)
Maisha ni shida na raha
Kuna starehe na karaha
Utachekwa ukizubaa

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI