MISTARI YA WIMBO HUU

Mimi ni dhahabu
Almasi

Labda nifungue Twitter na Facebook uone meseji zangu
Pengine utapata wivu wa mapenzi usinitese
Maana nimekuwa nyama baridi
Umeniweka kwenye jokofu jipya
Wanihifadhi kwa mapenzi ya baadae (baadae)
If you don’t love me now
Baby, nakushangaa
Uniweke wazi, na mapenzi bubu siwezi
Kila kikiisha kisa huja visa
Ni kisa kwa visa, yaani ni vita
Nakueleza ukweli wa moyo

Mimi ni dhahabu, mimi ni almasi
Usinitese tese ukidhani nitakosa
Mimi ni dhahabu, mimi ni almasi
Usinitese tese ukidhani nitakosa

Maulana kanjalia niwe na moyo wa heri nakusamehe
Mengine nayaona kwa mbali naigiza sioni
Laiti ungejua gharama yangu sidhani
Ungeninyanyasa nyanyasa na kunifanya nijidharau
Vingi sana nimekuza ndani ila hayabebeki
Ingekuwa ushindani, ninge-surrender
Mengi sana tumesameheana ila hauthamini
Umegeuza upole wangu ndio sababu ya kuniumiza

Wajua naeza fanya yangu unavyofanya yako
Na mi nisikusumbue
Shukuru marafiki zako wananipa moyo nikuvumilie

Mimi ni dhahabu, mimi ni almasi
Usinitese tese ukidhani nitakosa
Mimi ni dhahabu, mimi ni almasi
Usinitese tese ukidhani nitakosa

Wajua naweza fanya yangu unavyofanya yako
Na mi nisikusumbue
Wewe baby

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI