MISTARI YA WIMBO HUU

Ameen ameen ameen
Mungu niongezee
Ameen ameen ameen
Nishike mkono niongozee
Ameen ameen ameen
Mungu niongezee
Ameen ameen ameen
Nishike mkono niongozee

Ziende on and on kama Eryka Badu
Wafahamu sababu ni heshima kwa Mungu
Natembea kifua mbele yote sababu ya wewe
Wote wanaojipindua mwisho wanasanda wenyewe
Binamu yangu Masumbuko ananisikia hata akiwa jela
Jinsi nakinukisha na bado juhudi na sala
Naomba hekima za Suleiman sio miguvu ya bure
Hata kauli zangu ndogo zionyeshe nilienda shule
Maadui wafunge mikono nimewazidi wape ishara
Wape akili za hasara wachezee kazi na mshahara
Ikidunda sana inakaribia kupasuka
Yangu ikeshe isiishe leo hata wajukuu wanaikuta
Bora kuchekwa kuliko kuchekwa sana
Wanaonipinga waumize Mungu nakomba sana
Uwape umri mrefu wa kwangu na wa babu yangu
Ili roho zao ziumie wakiona mabalaa yangu
Amen

Ameen ameen ameen
Mungu niongezee
Ameen ameen ameen
Nishike mkono niongozee
Ameen ameen ameen
Mungu niongezee
Ameen ameen ameen
Nishike mkono niongozee

Nisichokijua hakiwezi kunisumbua
Wakisema mabaya yashindwe kunifikia
Wape kismati cha paka cha kupendwa na wachawi
Mi naomba cha pesa na kwa ujinga niwe kiziwi
Wape wanawake wazee na mafukara halafu wagonjwa
Ama mabwana mabwabwa wasiogonga kabla ya kugongwa
Wanaomba nisiwe na kitu ili niombe waninyanyase
Dhiki inijae vyote vya kwangu wavipate
Kuna viumbe hata huwajui na bado wana beef na wewe
Kama wanichukue msukule nisionekane wabaki wenyewe
Naishi kwa kudra baraka matakwa yako
Siwezi nikachemsha kama ukibaki upande nilipo
Competition is irrelevant with you by my side
Nafanya siongei na wanajua mi ni mastermind
Haraka zaidi yao uchungu zaidi yao
Ukubwa au udogo wa tatizo unaletwa na akili zao
It’s a wrap

Ameen ameen ameen
Mungu niongezee
Ameen ameen ameen
Nishike mkono niongozee
Ameen ameen ameen
Mungu niongezee
Ameen ameen ameen
Nishike mkono niongozee

Mi nna haraka zaidi yao
Pia hata uchungu zaidi
Rhumba likinipiga nazidi kukugeukia kwako Muweza
Pia hata uchungu zaidi
Rhumba likinipiga nazidi kukugeukia kwako Muweza

Ameen ameen ameen
Mungu niongezee
Ameen ameen ameen
Nishike mkono niongozee
Ameen ameen ameen
Mungu niongezee
Ameen ameen ameen
Nishike mkono niongozee

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU