MISTARI YA WIMBO HUU

Amekoma (amekoma)
Amekoma
Amekoma (amekoma)
Amekoma
Alidhani poa poa kumbe sio poa
Ah Side Mnyamwezi
Alidhani poa poa kumbe sio poa
Ah Side Mnyamwezi

Anaitwa Side Saidi Mnyamwezi mtoto wa Mbezi
Ni mtu wa kulipuka pamba ile kishenzi
Anamiliki Prado Corolla pamoja na Benz
Ni kijana mcheshi mtanashati ushauri huwa hataki
Matumizi yake kwa siku yanazidi laki
Mi namsimulia historia yake sababu nimekua nae
Huyu nimesoma nae mpaka sasa nishagombana nae
Wazazi walimshauri huyu akawa na kiburi
Alikuwa hana malengo wala dira kama tahira
Ni muongo mtu wa fiksi aliwaharibu mabinti
Hana mapenzi ya kweli analaghai wakina dada
Mwishowe aliwatelekeza bila kutoa msaada
Alikuwa mpenda sifa demu wake wa kwanza alikuwa Latifa
Penzi halikudumu sana miezi kadhaa wakaachana
Hii ilikuwa ni furaha kwake kashamaliza haja zake
Yule akaenda zake
Akaja akang’oa mwingine alikuwa ni demu wa rafiki yake
Ye hatambui hilo anahamishia tu kwake
Na juzi kafumwa gesti na mtoto wa dada yake
Tabia yake na mambo yake wengi hawakuipenda
Masela mtaani walishapanga dili wampige mawe
Wazee wamekaa vikao wanatamani wamuue
Huyu jamaa wanamuita kiwembe huwa habakizi demu
Mtaani alimpata Radhia tukajua anamchumbia
Kila siku anae kwenye gari wanakula raha za dunia
Alimgharamia mpaka tukajua anaoa
Kumbe maisha ya yule binti anaenda kuyatia doa
Radhia atake nini asipewe? Chochote kisichelewe
Utasikia nataka gari tulia ntakupa
Nataka simu usihofu ntakupa
Hii tabia sijui amerithi au amelogezewa
Anayoyafanya jamani nahisi ametumwa na shetani
Keshagombana na rafiki zake kisa wanawake
Side huyo

Amekoma (amekoma)
Amekoma
Amekoma (amekoma)
Amekoma
Alidhani poa poa kumbe sio poa
Ah Side Mnyamwezi
Alidhani poa poa kumbe sio poa
Ah Side Mnyamwezi

Side huyo Side huyo
Mnyamwezi huyu hapa tena
Akishamaliza anatema
Aliendelea na tabia yake ili afurahishe moyo wake
Alishapataga kesi ya kumtorosha mwanafunzi
Na hivi juzi juzi badala ya kung’oa demu kang’oa shoga
Kaenda kula kiboga bila uoga
Kwa tabia yake ya kishenzi alishindwa kuishi Mbezi
Akaja akahamia Chang’ombe akapata demu shombe shombe
Anakunywa pombe
Alimlea vizuri akamuhonga mpaka gari kwao akatoa mahari
Ni starehe juu ya starehe wanakula raha mazee
Kwa kuwa alikuwa nao wengi hakujua hamchukue yupi
Amuoe yupi
Alhamisi Ladies Free kama kawaida Bilicanas
Akaenda akang’oa mlupo alikuwa na rafiki zake
Akawatelekeza wenzake
Eti kisa demu ndo unawatelekeza masela
Aliondoka na huyo demu wakaenda kujipumzisha
Kumbe demu si demu demu mwenyewe anatisha
Popote utakapomfikisha lazima atalianzisha
Vimbwanga vilivyomkuta ilibidi Side adate
Wamefika gesti ndani picha linaanza demu jini
Anataka kumvua kimini demu kaanguka chini
Anataka kumsogelea mara demu kapotea
Anataka kumkumbatia demu kageuka kawa ngamia
Side anaanza kulia anatafuta njia ya kukimbilia
Binti anaanza kubadilika sura za ajabu ajabu
Mara Latifa mara Radhia mara Stella eh
Mara kageuka Rashidi ikabidi Side atoke nduki gesti uchi
Huku anapiga kelele kama mwizi au chizi
Walinzi wamemkosa kosa na mishale walijua mwizi
Yuko uchi wa mnyama popo angani wanamtazama
Anaita mama mama mama kimefika kihama
Ikabidi wangwana wamsitiri kwa kumpa nguo
Anaapa amekoma Chang’ombe nzima anaona noma
Wiki nzima hii hajatoka nje
Anaona aibu mambo yaliyomsibu
Side huyo Side huyo Mnyamwezi

Amekoma (amekoma)
Amekoma
Amekoma (amekoma)
Amekoma
Alidhani poa poa kumbe sio poa
Ah Side Mnyamwezi
Alidhani poa poa kumbe sio poa
Ah Side Mnyamwezi

Anauza sura Masaki
Anaishi ghetto Magomeni
Choo cha kulenga ugali tembele
Nyumba makuti Side Mnyamwezi
Wanaume walimwambia lakini wapi mchizi hakutaka kusikia
Kila nachomwambia lakini wapi mchizi hakutaka kusikia
Jibu lake (aah wapi)
Kwa machizi (aah wapi)
Kwa masela (aah wapi)

Amekoma (amekoma)
Amekoma
Amekoma (amekoma)
Amekoma
Alidhani poa poa kumbe sio poa
Ah Side Mnyamwezi
Alidhani poa poa kumbe sio poa
Ah Side Mnyamwezi
Amekoma (amekoma)
Amekoma
Amekoma (amekoma)
Amekoma
Alidhani poa poa kumbe sio poa
Ah Side Mnyamwezi
Alidhani poa poa kumbe sio poa
Ah Side Mnyamwezi

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI