MISTARI YA WIMBO HUU

Natamani, nikitaka lala
Basi nijilaze kifuani mwake yeye
Natamani, nikifumbua macho
Awe wa kwanza nione sura yake yeye
Alisema babu usimtusi mamba, hujavuka mto
Akasema bibi usidharau kijiko, ukipata mwiko
Wanaopenda usiwaone wazembe
Kukupenda usinione mi mzembe
Kama mapenzi pesa kwa kipato chako
Ningeondoka
Kama mapenzi raha kwa hizo kero zako
Basi ningechoka

Naomba Mungu uh
Nipate nafuu
Utulie kwangu
Maana ninakata kitunguu uh
Macho yako juu
Machozi kwangu

Angejua
Mimi ndo n’naejua thamani yake
Angejua
Asingedanganywa akaumiza moyo wake
Angejua
Mimi ndo n’naejua thamani yake
Angejua
Asingedanganywa akaumiza moyo wake

Kama pendo lingekuwa jangwa
Nami ngamia ningepita kimya
Ila yanachoma moyo, eh
Maumivu yangekuwa taa
Ningeshazima
Hasira tabu ya moyo, eh eh
Nasikia, sikia maneno tu mitaani
Na kila wakisema nahisi nasemwa mimi
Eti “ukiona umependwa basi jua
Mjinga katendwa”
“Ukiona umetendwa basi jua
Kuna mjanja kapendwa”
Sitajuta na sitalalama popote
Ntasema na moyo wangu (sema na moyo wangu)
Au labda, niulize tu Mola
Lipi fungu langu (fungu langu)

Naomba Mungu uh
Nipate nafuu
Utulie kwangu
Maana ninakata kitunguu uh
Macho yako juu
Machozi kwangu

Angejua
Mimi ndo n’naejua thamani yake
Angejua
Asingedanganywa akaumiza moyo wake
Angejua
Mimi ndo n’naejua thamani yake
Angejua
Asingedanganywa akaumiza moyo wake

Basi aseme
Kama nimekosea, anisamehe
Asiniteme
Maana naona mapema tuendelee
Basi aseme
Kama nimemkosea, anisamehe
Asiniteme
Maana naona mapema tuendelee

(Free Nation!)

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI