MISTARI YA WIMBO HUU

Anita (iye iyee)
Anita wangu (uwo uwo)
Lelele lilele iye iyee
Nasukuma sukuma, ili siku ziende
Urudi nyumbani tuishi pamoja

Nasikia mazoea yanatabu, leo ndio naamini
Tangu uondoke Anita raha nakosa mimi
Hukumbuki tulilishana yamini
Kwamba mimi na wewe
Maisha milele mpaka nafukiwa chini
Ni mawazo yanautesa moyo wangu Anita nielewe iyee
Natamani uyajue ili unilinde mimi
Sijajua uliwaza nini Anita kuwa mbali na mie iyee
Hata hilo nilijue ili nisaishwe mimi
Kama ni maradhi, mimi ndio wako dakitari
Unambie mapema ili dawa yake niijue
Ama ni waradhii iiih hiii
Anii..

Anita (iye iyee)
Anita wangu (uwo uwo)
Lelele lilele iye iyee
Nasukuma sukuma, ili siku ziende
Urudi nyumbani tuishi pamoja

Unajua mi nilikupendaa zaidi
Ila ya dunia we yalikuzidi
Nilitamani kuwa nawe zaidi
Kuliko yoyote unayemdhani
Siku zote uko safarini kuniacha mimi upweke
Mi nilikupenda sana we mpenzi
Je kweli wataka kunienzi?
Au unataka kunitia mi mashakani?

Siku zaenda kama chizi, ni yangu njiani naongea
Hiyo yote sababu yako Anita kilio pokea
Chefu na majirani mtani wanakuulizia
Sina la kuwajibu nabaki kama chizi najililia
Waliniambia nikuache wewe
Ili mi niishi mwenyewe
Masikio nikaziiba, vipi niishi bila wewe
Wakasema hutonithamini, wala haikuniingia akilini
Mbuzi gita wakapiga jua wewe ndio wa maishani
Anita wewe umeumbika mama
Kila upitapo nyuma lawama
Sijiwezi mtoto wa kitanga
Kwako taabani nishabwaga manyanga
Anita wewe umeumbika mama
Kila upitapo nyuma lawama
Sijiwezi mtoto wa kitanga kwako taabani
Anita, nakuita..

Anita (iye iyee)
Anita wangu (uwo uwo)
Lelele lilele iye iyee
Nasukuma sukuma, ili siku ziende
Urudi nyumbani tuishi pamoja
Anita (iye iyee)
Anita wangu (uwo uwo)
Lelele lilele iye iyee
Nasukuma sukuma, ili siku ziende
Urudi nyumbani tuishi pamoja

Pamoja, pamoja na Dunga
Ndani ya 41 Records
Pamoja iih na Jide (aan haa, ah Jide)
Mkata
Ndani ya 41 Records (oh pamoja)

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI