MISTARI YA WIMBO HUU

Namtafuta kote alipo
Aseme kama nilimuudhi
Aseme kama nilimkosea
Aseme kama amenisamehe
Namtafuta kote alipo
Aseme kama nilimuudhi
Aseme kama nilimkosea
Aseme kama amenisamehe

Peke yangu najiongoza
Kwenye milima mimi napanda
Kwenye mabonde mimi nashuka
Makorongo Q naruka
Kwenye jangwa la ufukara
Chozi yangu ndio maji yangu
Jua linanichoma
Mvua inaninyeshea
Ndugu wamenitenga
Maadui wamenizunguka
Moyoni namuombea
Ipo siku tutaonana
Machozi yananitoka
Hakuna wa kunifuta
Mama uko wapi?
Mama uko wapi?

Namtafuta kote alipo
Aseme kama nilimuudhi
Aseme kama nilimkosea
Aseme kama amenisamehe
Namtafuta kote alipo
Aseme kama nilimuudhi
Aseme kama nilimkosea
Aseme kama amenisamehe

Malaika nawatuma
Mwambieni nampenda
Mwambieni sijamtenga
Hakuna neno zuri kwake
Kama neno ‘nampenda’
Rafiki zake hawajanitenga
Ila mumewe amenitenga
Takadiri siwezi epuka
Nasubiri litalonifika
Mwambieni nampenda
Mwambieni sijamtenga
Mwambieni nampenda
Mwambieni sijamtenga
Mwambieni nampenda

Namtafuta kote alipo
Aseme kama nilimuudhi
Aseme kama nilimkosea
Aseme kama amenisamehe
Namtafuta kote alipo
Aseme kama nilimuudhi
Aseme kama nilimkosea
Aseme kama amenisamehe

Peke yangu najiongoza
Kwenye milima mimi napanda
Kwenye mabonde mimi nashuka
Makorongo Q naruka
Kwenye jangwa la ufukara
Chozi yangu ndio maji yangu
Jua linanichoma
Mvua inaninyeshea
Ndugu wamenitenga
Maadui wamenizunguka
Moyoni namuombea
Ipo siku tutaonana
Machozi yananitoka
Hakuna wa kunifuta
Mama uko wapi? Mama uko wapi?

Namtafuta kote alipo
Aseme kama nilimuudhi
Aseme kama nilimkosea
Aseme kama amenisamehe
Namtafuta kote alipo
Aseme kama nilimuudhi
Aseme kama nilimkosea
Aseme kama amenisamehe

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI