MISTARI YA WIMBO HUU

Kutwa kidomo wazi
Nikifuta na machozi
Huku namuomba Mola unitoke moyoni
Ila ndo siwezi
Nakesha ka mlinzi
Maana hata nkilala unaniijia ndotoni
Bado
Asante kwa kuniumiza
Nimejifunza mengi mwanzo sikuyajua
Katu
Naapa kutolipiza
Na mwambie mapenzi abaki kuyasikia

Nakumbuka maneno yako
Hutonikimbia
Utabaki nami
Tena ukala na viapo
Taurati Bibilia
Leo sikuoni

Ila mwenzako bado
(Bado bado)
(Bado bado)
Mwambie bado
(Bado bado)
(Sijapona)
Ila mwenzako bado
(Bado bado)
(Bado bado)
Mmh bado
(Bado bado sijapona)
Sijapona roho

Aa-ah Mola
Nishike mkono Baba Muumba
Haya ninayoyaona simanzi
Ah yaani bora
Jicho mchanga ningefumba
Huenda ningeshapona maradhi
Oh maumivu yangu
Hayawezi kupona kwa vidonge
Sababu panaponichoma nkipapasa sipaoni
Kweli peke yangu
umeniacha na unyonge
Kabisa wakanipokonya tonge langu mdomoni

Nakumbuka maneno yako
Hutonikimbia
Utabaki nami
Oh mi ndo mwili mi roho yako
Yaani umetimia
Mbona sikuoni

Ila mwenzako mimi
(Bado bado)
(Bado bado)
Mwambie bado
(Bado bado)
(Sijapona)
Ila mwenzako bado
(Bado bado)
(Bado bado)
Mmh bado
(Bado bado sijapona)
Sijapona roho

Ile roho yangu mama
(Ibebe)
Inandondoka
(Ibebe)
Iokote mama
(Ibebe)
Chaukucha nsije zima
Uh roho yangu
(Ibebe)
Inandondoka
(Ibebe)
Njoo unshike mama
(Ibebe)
Chaukucha nsije zima)
Ah aah ai wewe
(Ibebe)
Watanizika mama
(Ibebe)
Mwenzio taabani
(Ibebe)
Chaukucha nsije zima

Masikini pendo langu
(Ibebe)
Linandondoka
(Ibebe)
Niokote mama
(Ibebe)
Chaukucha nsije zima

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU