MISTARI YA WIMBO HUU

Naitwa Fareed
Kwa maana mie ni wa kipekee na wa aina yake
Huu ujasiri na huu utajiri wa mashairi una tafsiri zake
Jasiri coz siogopi kuumia
Nikiwa na noti hutumia
Akina kidoti wakiniaproach huwakazia
Tajiri wa mashairi mie sio hodari wa kurap tu
Mie sio msanii naifanya hii kwa ajili ya watu
Nina uso wa mbuzi na ninapewa front page
Na daily kwenye news sina skendo yoyote
Wapi wapi wapi wapi niliwakosea
Wapi mie siku-play fea (fair)
Sikuzaliwa niwe kamili nilizaliwa niwe real yeah
Na udhaifu hauna dili ikiwa ni strong najifeel here
Nadhifu kiakili street smart black Shakespeare
Nipo ili nife maisha sio mchezo wa uwoga mjomba
Unataka nishibe hakikisha haukombi mboga bomba
Nipake tope nijikombe nikuombe mafuta
Unipond eunizonge kutwa nikonde mnyonge wa kutupwa
Kwa mgongo wa chupa nipake nisije kupauka
Nitaibuka tu kama vumbi dongo likija kukauka

Ninateleza nakosea naanguka napotea
Najifunza kuendelea ninainuka natembea
Nateleza nakosea naanguka napotea
Najifunza kuendelea ninainuka natembea
Bendera ya chuma
Inapepea
Bendera ya chuma
Bendera ya chuma
Inapepea
Bendera ya chuma

Ninachunga hasira isiniumize ili maumivu yasinitishe
Hawaishi hila wenye wivu wananizingira nisipite
Dua haziishii angani
Ua linazaa bustani
Bahati haina ahadi ikihitaji hutua ndani
Sihofii kudondoka sababu mie nina mabawa
Waliofikiria nitachoka wanaogopa Ngosha ana power
Cheusi ni mzawa Cheusi ana dawa ya kutoka
Pagawa ukinitosa Kosa kunawa kabla haijatosha
Kivipi uniache wakati huu mziki uko na mie
Na kwake nina mapenzi ya mswaki
Sitaki mwingine achangie
Masika bila mbu sio gharika bila nuuh
Shida anazo kila mtu chakarika uje unafuu

Hekima ni kukosa excuse (kukosa excuse)
Unapo loose
Na pia ukishinda usijiboost (usijiboost)
Ya nini makuzi
Hekima ni kukosa excuse (kukosa excuse)
Unapo loose
Hekima ni kukosa excuse (kukosa excuse)
Unapo loose

Ninateleza nakosea naanguka napotea
Najifunza kuendelea ninainuka natembea
Nateleza nakosea naanguka napotea
Najifunza kuendelea ninainuka natembea
Bendera ya chuma
Inapepea
Bendera ya chuma
Bendera ya chuma
Inapepea
Bendera ya chuma

Ninawafanya wanakaa kama yule MC wa Kenya
Ukisikia paa ujue haikupangwa ufe mapema
Sikuiti shujaa kwa kufanya kile unachofanya
Nitakuita mjinga ikiwa ukishindwa wakati chawezekana
Dunia ni kubwa pia ni ndogo kama tukiungana
Kiutuuzima Na mlima haupandwi kwa kuutazama
Ningekua kisiwa maisha yangu yangekua ufukweni
Huu upeo nimetunukiwa na Mungu wangu basi nipokeeni
Inatosha wanasema ‘ hapana ‘ dondosha
Na tena wanaochana hawajiiti conscious ni Ngoshaz

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU