MISTARI YA WIMBO HUU

Yoh yoh yoh
Ndani ya Bongo mambo super hapana ubongo
Ingawa sometime Bongo chungu kama sifongo
Nafanya makaratee kama machinga mtaa wa Kongo
Kimtindo mtindo nakata ngebe vimtima nyongo
Hapana matata kitu roho inapenda mtapata
Bongo Dar Es Salaama ni mpeto wa kutakata
Nenda viwanja vikali vya Bongo ustaajabu
Na pita Sleepway, Blue Pam au Mambo Club
Kama hujazoea unaweza ukavunja shingo
Mambo Isidingo watu mkononi Nokia bingo
Huwezi kujua yupi mtoto wa geti, yupi changu
Wote wanameremeta kama mamtoni mwanangu
Hizi zinapoyeyuka wabongo tunalia ukata
Subiri kichapo chake pale mbongo anapozipata
Mwendo wa kiti kirefu jirani na nyama choma
Na toto mbili tatu za geti au za kona
Hii watu wa Bongo tunasema napoteza mawazo
Lakini mara nyingi hutokea wakati unazo
Wakati wa dumba kali saa moja shuka utosini
Na kujifanya unawaza mambo mengi ya ofisini
Pitia pitia night kali mitaa ya Kinondoni
Kina dada poa nusu uchi fegi mdomoni
Na kama una gari watajazana madirishani wee
Mpaka ukose hewa wote wanataka hisani
Kwenye madaladala kuibiwa ni kawaida
Vaa cheni shingoni, saa mkononi utoe faida
Wacha dirisha wazi kisha ukatize Manzese
Ili uwape mateja mtaji waende chimbo wakatese
Rudi Mwananyamala oh! Mateja kibao
Katiza saa moja moja uone roba za mbao
Utaona kama mtoa roho yuko karibu yako
Ni kheri utoe chochote ili uokoe nafsi yako

Bongo eh
Bongo Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Bongo Dares Salaam
Kaa chonjo eh
Ndani ya Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Ndani ya Dares Salaam

Bongo ya sasa sio ya mwaka 47
Mpaka bibi vizee sasa wanafanya ukahaba
Sijui niseme nini ili muweze kunielewa
Na sijui nifanye nini nisaidie wanaoonewa
Hakuna heshima, ni vurugu mechi kwenye jamii
Hakuna utii wala mafunzo ya manabii
Na wezi wa mfukoni wanachomwa moto kinyama
Mwingine hajaiba kapewa kesi kwa uhasama
Nani atakae jua na sheria ipo mikononi?!
Watu wa Bongo mbona hamna utu moyoni
Vijana wamejibana wapate mtaji wa biashara
Nawaita machinga ingawa sio wote kutoka Mtwara
Mbaya kuliko vyote mnapovunja vibanda vyao
Wengine walikuwa wezi, je warudie zama zao?
Ni mshike mshike sometime ni vita na mapolisi
Wao na sisi, rungu na pingu kama ibilisi
Huku kwetu uswahilini ni mambo ya kila siku
Na ni kama kuibiwa cheni kwenye ngoma za mchiriku
Wabongo wanapenda sana starehe kuliko kazi
Wanatamani wangezaliwa Blue Nay wamwage radhi
Masista duu wa Bongo wanazidi kupanda chati
Huwezi kujua yupi wa Kigogo, yupi wa Masaki
Mablaza majina yao ya asili hawayataki
Bitoz Nyangema anataka aitwe Tupac!
Ni burudani tosha, hivyo ni vijimambo tu
Wabongo tuna title kubwa lakini hatuna kitu
Unaujua mstakabari wa ma-superstar wa Bongo?
Lazma ufunzwe chuo kikuu cha mbwembwe za uongo
City center, ofisi ni mtu aliposimama
Hata muhuri wa ikulu unapata haina gharama
Ngoma inakuwa nzito mnapokutana matapeli
Akili kumkito ukilemaa umeachwa ferry
Aliyeuziwa cheni katoa hela bandia
Aliyepokea hela nae kauza cheni ya bandia
Tuliozoea jiji tunasema ngoma droo
Na una-set mambo mengine yaende kwenye mtandao

Bongo eh
Bongo Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Bongo Dares Salaam
Kaa chonjo eh
Ndani ya Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Ndani ya Dares Salaam

Katikati ya jiji hata usikiri dili haziji
Na ukitaka ku-win Bongo cheza dili na wale magwiji
Naona vijana wa Bongo wanapenda safari kafiri
Hata mkoba wanategua kitendawili
Safari bado ni ngumu jamani msiende kwa nguvu ya ndumba
Ujinga sumu acha Mwenyezi awahukumu
Changa uchange uende kiwanja unachotaka
Funga mkanda, fungua mabano unavyotaka
Maskani Kimara, watu kila siku magoni
Jonas Kiwia wasalimie Washington
Ukiweza pita Texas mpe hi Chief Son
Na mkumbushe uzushi wa Bongo Dar es Salaam
Sinza ya leo, kila baada ya nyumba bar
Na zote zinajaa, hapo ndipo utakaposhangaa
Na kwenye night club ni lundo la kaka poa
Huwezi ukaamini jinsi walivyojipodoa
Upinzani wa jadi Bongo haupo Simba na Yanga
Matonya na Makamba, na Sitte na wamachinga
Na kali kuliko zote upinzani konda na denti
Wanaposhika mashati tu denti anapoketi
Hakuna mnyonge, wala anayekubali kushindwa
Ngoma ngoroigwa na wote wanataka ubingwa
Na watu wana magari mpaka ya milioni 200
Kwa mbongo wa kawaida baiskeli kitendawili
Wasioamini ni wale wenzangu na mimi
Mlio na imani iliyopo juu mngoje chini
Mtangoja milele, na mtakufa bila kelele
Kama walivyokufa wafuasi wa Kibwetele
Ndani ya Bongo!

Bongo eh
Bongo Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Bongo Dares Salaam
Kaa chonjo eh
Ndani ya Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Ndani ya Dares Salaam

Bongo eh
Bongo Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Bongo Dares Salaam
Kaa chonjo eh
Ndani ya Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Ndani ya Dares Salaam

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI