MISTARI YA WIMBO HUU

Kusuka au kunyoa
Kuwa na mkono wa birika au wa kutoa
Kujenga taifa au kubomoa
Kufunga pingu za maisha au kukataa kuoa
Kugawanya kujumlisha kuzidisha au kutoa
(Chagua moja)
Uishi kihuni au kifala
Ufanye mziki spoon au ufanye mziki biashara
Iwe Katuni au Hip Hop imara
Chagua kuchuna au kuchonga ngenga
Ukatwe suna au ubakie na mkono wa sweta
Usahau ya nyuma uangalie unapokwenda
Ufanye kazi kama mtumwa ili uje uishi kamfalme
Usimame au ukae
Umchukie au umpende akupendae
Ufiche uchi
Au uvue chupi uzae
Unipe heshima yangu au niichukue kwa nguvu
Nijifanye na adabu au nikuletee ukauzu
Chagua moja

Mshika mbili siku zote moja humponyoka
Kusuka au kunyoa bado vyote we unataka
Mshika mbili siku zote moja humponyoka
Kugawanya kuzidisha jumlisha au kutoa

Nasimama nimeshachoka mi kukaa juu ya kiti
Kivipi sipiti
Nipe beat niidhibiti
Upeo wangu unaona mbali na bado natafakari
Sikiliza yangu mistari yenye ukali wa tindi kali
Chagua moja
Kuimba ama kuchana
Wapo wengi wanaimba ingawa topic hazina maana
Chagua moja
Uwe mpole ama mtundu
Uwe msomi ama mbumbumbu
Uishi Manyoni ama Kemundu
Kwetu moja kati yake sawa
Ili mradi maisha uyamudu
Chagua moja
Ujiunge CCM au CUF
Ung’atwe na nyigu au siafu
Ukutane na jini au wafu
Chagua moja
Ukutane na mabaya au mema
Kumeza ama kutema
Kunyamaza ama kusema
Amua kati yao
Umuoe mweupe au mweusi
Usambaze ujumbe au kirusi
Bahati au nuksi
Ubinadamu ujasusi
Ama uhutu na utusi
Chagua moja
Unyongwe uzikwe hai
Tumia zana kwenda dry
Kuvaa beli na jeans au mwichi mwichi unyonge tai
Chagua moja (ah)
Kuhonga ama ku-tip
Kupiga ama ku-beep
Majangwa ama misitu mi kwangu si mali kitu

Mshika mbili siku zote moja humponyoka
Kusuka au kunyoa bado vyote we unataka
Mshika mbili siku zote moja humponyoka
Kugawanya kuzidisha jumlisha au kutoa

Haya maneno dhahiri hii hoja si ya kuokota
Mshika mawili siku zote moja humponyoka
Hata ukifanya kosa ukaamua kuongopa
Chagua moja
Sio unajishtukia unagota
Kugangamara na kusota ili kutoka
Au kulala na kuota kuwa unafoka
Chagua moja
Kuamua kungoja
Au kutumia kinga kwa kila tendo moja
Chagua moja
Kuchukua ama kuacha
Anasa
Ngono na ndoto za alinacha
Kudata
Au kuwa mzima yaani swadakta
Chagua moja
Kusali au kusaliwa kukubali kukataliwa
Kushikwa ama kuachiwa kutoka au kubakia
Chagua moja
Kushuka ama kupanda kikapu ama kandanda
Chagua moja
VCD au DVD Cinema ama TV
Starehe au kazi girlfriend ama wifie
Chagua moja

Mshika mbili siku zote moja humponyoka
Kusuka au kunyoa bado vyote we unataka
Mshika mbili siku zote moja humponyoka
Kugawanya kuzidisha jumlisha au kutoa

Chagua moja
Chagua moja
Chagua moja
Chagua moja
Chagua moja
Chagua moja

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU